Wakati wadau na wapenda soka barani afrika wakielekeza macho na maskio yao nchini Misri kwenye michuano ya kombe la Afcon inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni, kumezuka gumzo mitandaoni juu ya muonekano wa nyota wa ‘Harambee Stars’ ya Kenya mwenye umri wa miaka 26, Joash Onyango

joash onyango

Picha hii imezua taharuki hasa kutokana na muonekano wake ukilinganisha na umri ni vitu viwili ambavyo katika hali ya kawaida haviendani, Joash ni mzaliwa wa Januari 31 mwaka 1993 nchini Kenya akiwa na jumla ya miaka 26.

Beki huyu wa timu ya taifa ya Kenya anaitumikia klabu ya Gor Mahia huku akiwa nchini Misri katika michuano ya Afcon anatarajiwa kukutana na mshambuliaji hatari wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane mwenye umri wa miaka 27 pamoja na Mbwana Samatta anayekipiga timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwakuwa katika kundi moja kwenye michuano hiyo.

Klabu yae ya Gor Mahia wamethibisha kuwa ni mchezaji wao “Tunathibitisha kuwa picha hizo ni kweli za mchezaji wao, Joash Onyango ambaye yupo kwenye majukumu na timu ya taifa. Na watu wasimlinganishe na mtu mwingine katika eneo la ulinzi wa timu hiyo ya taifa ya Harambee Stars AFCON 2019 Misri.” Gor Mahia wamethibitisha

Joash Onyango amezua taharuki akiwa kwenye maandalizi ya michuano hiyo ya Afcon huku wengine wakimlinganisha muonekano wa beki huyo wa Gor Mahia sawa na ule wa aliyekuwa nyota wa Senegal, El Hadji Diouf na Rigobert Song wa  Cameroon.

Walichoandika kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya picha ya beki huyu wa Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya kuonekana

Source link