Wakati huo, alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa na mfanyakazi wa kampuni ya ndege mjini Delhi.

Salla aliripotiwa kuwa alimuomba mpenzi wake ahamie Mumbai lakini alikataa, na kwa kuichafulia sifa kampuni ya ndege , alitumai angepoteza kazi na kulazimika kuishi nae.

Mchunguzi wa tukio hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba japo Salla hakufanya utekaji wowote , kitendo alichokifanya cha kuweka waraka wenye vitisho bado kinamtia hatiani kwa kosa kujaribu kuiteka ndege kwa mujibu wa sheria ya India.

Marubani wa ndege hiyo watapokea kila mmoja Rupia 100,000 kutoka kwenye fidia atakayoitoa kwa “mkanganyiko walioupata ,” aliamuru jaji. Kila mhudumu wa ndege pia atapokea Rupia 50,000 r , na kila msafiri atalipwa Rupia 25,000.

Wakili wa Salla , Rohit Verma, alisema kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.

Jet Airways, ambayo wakati mmoja ilikuwa ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini India, iliahirisha safari zake zote za ndani ya nchi na za kimataifa mapema mwaka huu baada ya kupata matatizo ya kifedha.Source link