Dr Alphonse Rugambarara

Katika Mfululizo wa makala maalum kuelekea kombe la afrika la mataifa nchini Misri ,tunaangazia timu ya taifa ya Burundi.

Mwanzilishi wa timu hiyo Dr Alphonse Rugambarara anasema mafanikio ya timu hiyo yametokana na mfumo waliouweka ilipoanzishwa mwaka 1990 ,kwa kutengeneza vipaji na kutoa mafunzo kwa makocha wazawa ,hali iliyoifanya Burundi kuwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kushiriki kombe la dunia la vijana.Katika kombe la mataifa Afrika Burundi itacheza mechi zake katika kundi linalojumuisha pia Nigeria,Madagascar na Guinea

Dr Alphonse Rugambarara amemueleza mwandishi wa BBC Yves Bucyana jinsi timu ya taifa ya Burundi ilivyoanzishwa mwaka wa 90 wakisaidiwa na taifa la Gabon

”Federation ya Gabon ilitusaidia kujenga timu kabla ya 1990 hatukua na timu ya taifa, tukaenda Gabon tukaifunga Gabon, hiyo ilituinua sana kisha tukaandikishwa kuingia kuwenye michuano ya CAF”

Anasema mafanikio ya Burundi yametokana hasa na kuwajali vijana na makocha wazawa na hawakukawia kupata matunda,Burundi ikawa nchi ya kwanza afrika mashariki kutinga fainali za kombe la dunia la vijana waliochini ya umri wa miaka 20 mwaka 1995.

Wachezaji waliotemwa Kenya na Tanzania wazua minong’ono

Wakati huo Dr Rugambarara ndiye alikuwa mkuu wa chama cha soka cha Burundi kabla ya kuwa waziri wa michezo wa nchi hiyo.

Nchini Misri Burundi itapiga mechi ya kwanza dhidi ya Nigeria katika kundi linalojumuisha pia Madagascar na Guinea. ana matumaini kuwa timu ya Intambamurugamba itafanya vyema.

”Timu yetu ni nzuri, wachezaji wengi wanacheza katika nchi ambazo mpira wa miguu uko juu walishapata uzoefu wa michuano na kujua michuano nini na mpira ni nini, nchi ambayo itakua changamoto kwetu ni Nigeria”.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Timu ya Burundi itategemea sana uzoefu wa mshambuliaji Saido Berahino

Timu ya Burundi itategemea sana uzoefu wa mshambuliaji Saido Berahino,lakini hivi karibuni timu ya Stoke City ilisimamisha mkataba wake kutokana na utovu wa nidhamu,jambo linaloweza kuathiri mchezo wake na timu nzima kwa ujumla.Dr Rugambarara atoa ushauri wake:

”Mtu mmoja hawezi kuendesha timu yeye mwenyewe, nachoweza kusema ni kuwa awe na nidhamu, ni bidii yake ambayo itamfanya afanye vizuri kwenye timu yake, vinginevyo asipozingatia suala la nidhamu ni vigumu kuendelea vizuri”.Source link