Abiy AhmedHaki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kamati ya tuzo ya Nobel imesifu jitihada za Waziri Mkuu Abiy

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Abiy Ahmed ametikisa Ethiopia tangu alipokuwa Waziri Mkuu mnamo mwezi Aprili mwaka jana, lakini je ni mawazo ya aina gani yyaliyojikita kwa bwana Abbiy aliyepata tuzo Jumanne huko Oslo?

Neno Medemer limekuwa maarufu sana nchini Ethiopia.

Neno hilo kwa lugha ya Kimhara linamaanisha ”kuongeza” lakini pia linatafsiriwa kama “kuja pamoja”, hali ambayo inaelezea jinsi waziri mkuu Abiy anavyoshughulikia changamoto zinazoihusu Ethiopia kwa njia ya kipekee.

Neno hilo aidha limekita mizizi baada ya waziri mkuu kuandika kitabu kilicho na neno hilo kilichozinduliwa katika hafla ya kufana mwezi oktoba katika miji tofauti nchini Ethiopia.

Inaripotiwa kuwa maelfu ya nakala za kitabu hiki zimechapishwa katika nchi hiyo ambayo lugha zinazozungumzwa zaidi ni Amharic na Afaan Oromoo.

Image caption

Medemer ni kitabu kilichochapishwa kwa lugha ya Amharic na Afaan Oromoo

Katika kitabu hiki chenye sura 16 na kurasa 280, Abiy anaangazia maono yake anayosema yamekuwa mwongozo wa maisha yake tangu akiwa mtoto.

Bwana Abiy anataka Ethiopia iwe na mshikamano wa kitaifa licha ya kwamba inakabaliana na mgawanyiko wa kikabila lakini pia anataka tofauti iliopo iwe yenye kufurahiwa na kila mmoja.

Mafanikio yake katika kuhakikisha linafanikiwa itakuwa jambo la msingi katika muda atakaokuwa madarakani.

Madhumuni ya ‘Medemer’ ni nini ?

Kitovu cha falsafa hii ni dhana ya kwamba, watu wanaweza kuwa na maoni tofauti lakini maridhiano yakapatikana.

Tangu alipoingia madarakani, ni wazi kwamba uongozi wa Bwana Abiy umekuwa tofauti kabisa na uliokuwepo katika kipindi cha miaka thelathini iliyopita.

Amejitahidi kuondoa msimamo mkali katika masuala ya kiusalama na kukumbatia njia za mazungumzo ya uwazi na kwa uhuru katika siasa.

Amesema kwamba watangulizi wake walijaribu kutumia mbinu za usawa na kupitisha kila kitu katika serikali kuu kuhusu masuala ya kiuchumi lakini wakashindwa kwa sababu ukosefu wa uelewa mzuri wa Ethiopia.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Tangazo la Abiy kama mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Oktoba, lilikuwa taarifa kubwa Ethiopia

“Tunahitaji kujitawala na falsafa ya Ethiopia ambayo msingi wake ni wa kawaida tu inayoweza kutatua matatizo tuliyonayo na kutuunganisha sisi sote”, ameandika katika kitabu cha Medemer.

Anasema kwamba maadili ya Ethiopia yanazingatia kujuimswa kwa kila mmoja na mshikamano

Wakosoaji wake wanasema kwamba jambo hili likaonekana kuwa zuri kupita kiasi machoni mwa watu, halitoi suluhu ya njia ya vitendo kuhusu namna ya kusonga mbele ama mwongozo wa kuweza kufikiwa kwa maridhiano.

Aprili, mchambuzi wa kisiasa Hilina Berhanu alisema kwamba medemer kimeeleweka vizuri na kuwa kama dawa ya maumivu kwa kile kilichotokea awali, lakini hakina mwelekeo wa siku za usoni.

Kwanini Abiy alishinda Tuzo hii?

  • Umauzi wake wa kutatua mgogoro wa mpakani na majirani zake Eritrea
  • Alianzisha mabadiliko muhimu ambayo yamewapa raia wengi matumaini ya kuwa na maisha bora ya baadaye.
  • Pia ametoa hakikisho la kuimarisha demokrasia
  • Amehusika katika majadiliano mengine ya kuleta amani na maridhiano nchini Ethiopia.

Waziri mkuu wa Ethiopia ashinda tuzo ya amani ya Nobel

Tamasha la Irreecha lasababisha msongamano Ethiopia

Lengo la Abiy kuanzisha wazo hili ni lipi?

Bwana Abiy alianza kuzungumzia medemer kabla ya kuwa waziri mkuu.

Akihudumu katika nyadhifa za juu serikalini, alikuwa akitumia neno hilo wakati anawaelezea wafanyakazi wenzake uhumimu wa kuleta mawazo mapoja na kuhamasisha watu kufanyakazi kwa mshikamano.

Kama waziri mkuu, alisema medemer inaweza kuwa tiba kwa wengi tu kuanzia matatizo ya umaskini hadi migogoro ya kikabila.

Alitaka watu kushikamana wakiwa na maono yanayofanana badala ya kujikita katika migawanyiko ya kikabila na kisiasa iliyokuwepo kwa muda mrefu.

Je kitabu cha medemer kinazungumzia nini kuhusu ukabila Ethiopia?

Kwa kiasi fulani kuna kejeli kwa maana kwamba waziri mkuu amezungumzia umoja wa kitaifa, na mabadiliko yake ya kisiasa yamezidisha wasiwasi wa kikabila nchini humo.

Katika kipindi cha miezi 20, ghasia za kikabila zimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuhama makazi yao.

Pia unaweza kusoma vile Ethiopia imebadiliko chini ya Abiy:

Ethiopia yamaliza uhasama na waasi wa OLF

Mageuzi yalivyoibua uhasama wa kikabila Ethiopia

Katiba ya Ethiopia iliandikwa mwaka 1995 kwa misingi ya kikabila ambayo iambayo inazingatia ukabila katika utekelezaji na kukosa kujumuisha mengine muhimu kama usawa na matabaka ya kiuchumi, Abiy amesema.

Lakini pia ametambua ukosefu wa haki ambao umekuwepo katika historia ya Ethiopia dhidi ya baadhi ya makundi ya kikabila kama miongoni mwa sababu ambazo huenda zinachochea ongezeko la wasiwasi nchini humo.

Waziri Mkuu mbaye anatoka kabila la Oromo, aliingia madarakani baada ya jamii ya waoromo kufanya maandamano wakilalamikia kutengwa kiuchumi na kisiasa.

Hata hivyo, medemer inatoa wito kwa makabila mbalimbali kujitokeza na kusherehekea kwa pamoja kama nchi.

Bwana Abiy anasema ukabila unaweza kwendana na uraia na kujikita katika haki za binafsi.

Lakini vile hili linaweza kufikiwa bado ni fumbo.Source link