Mwili wa Mfanyabiashara Ali Mufuruki umeaagwa leo Disemba 10, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, baada ya mwili wake kuwasili jana kutokea Afrika Kusini.Mamia ya Waombolezaji walijitokeza katika Ukumbi huo leo wakati mwili wa Mfanyabiashara maarufu nchini, Ali Mufuruki ukiagwa.


Mwili wa Mufuruki uliwasili nchini jana jioni ukitokea Afrika Kusini alipofariki na baada ya kuagwa leo utazikwa katika Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar.

Viongozi, Wastaafu, Wafanyabiashara na Wananchi wamejitokeza kumuaga Mfanyabiashara huyo ambaye kwa namna moja au nyingine aligusa maisha ya watu wengi.

Mbali na hao pia Balozi wa Marekani nchini Tanzania alishindwa kuongea baada ya kupewa nafasi ya kutoa salamu zake za rambirambia.

Mufuruki aliyezaliwa Novemba 15, 1958 amekuwa Mwenyekiti na Mjumbe wa zaidi ya bodi 30 za Kampuni mbalimbali katika kipindi cha miaka 25.

Alifunga ndoa na Bi. Saada Ibrahim Aprili 16, 1993 na kujaaliwa kupata watoto wanne ambao ni Laila, Zahra, Sophia na Tegegne.

 Source link