Beyoncé describes her latest project as "sonic cinema".Haki miliki ya picha
Paul Warner/Getty Images

Image caption

Beyoncé aliita Albamu yake “Barua ya upendo kwa Afrika”

Baadhi ya wanamuziki nyota zaidi barani Afrika wanatazamia kupata mafanikio makubwa kwa kiwango cha duni baada ya kuchaguliwa na l namwanamuziki wa Marekani Beyoncé kwenye albamu yake inayotia hamasa ya Lion King

Huku wanamuziki nyota wa Nigeria kama Wizkid na Burna Boy tayari wameweza kupenya katika nchi za Uingereza na Marekani , kolabo yao na Beyonce katika The Lion King: The Gift inatarajia kuinua kw akiwango cha juu kazi yao

Albamu hiyo yenye miziki 14- iliyokusanywa na Disney imefaa sati za muziki ambao umekuw amaarufu sana katika bara la Afrika . Beyoncé, ambaye alitunga, kuongoza na kuzalisha mradi wa muziki wake alliita ablbamu yake “Baruaya upenzo kwa Afrika”.

“Nilitaka kuhakikisha tunapata vipaji bora kutoka Afrika, na sio kutumia tu baadhi ya sauti au utfafanuzi wangu tu juu yake ,”aliliambia shirika la habari la ABC News.

“Nilitaka iwe na uhalisi kwa kile kilicho kizuri kuhusu muziki wa Afrika .”

Alitumia maneno katika lugha za Kiingereza, kiswahili, Pidgin English, Zulu, Xhosa na Yoruba, mradi wake ulijumuisha ladha mbali mbali za muziki kutoka Afrika kuanzia Afrobeats, pop, R&B, hip-hop, na sehemu ya ladha ya muziki wa Afrika Kusini unaofahamika kama Gqom.

” Ngoma nyingi, nyimbo hizi zote zikiwa na mchanganyiko wa sauti mpya za kuvutia kwa ushirikiano na baadhi ya maprodyusa kutoka Marekani ,ytuliweza kubuni aina yetu ya muziki “, Beyoncé aliliambia shirika la habari la ABC.

Wanamuziki wa kiafrika walioshiriki kwenye albamu hiyo walikuwa ni pamoja na Tekno, Yemi Alade, Mr Eazi na Tiwa Savage, pamoja na mwanamuziki wa Cameroon Salatiel, na wa Afrika Kusini Busiswa na Moonchild Sanelly. maprodusa kadhaa wa kiafrika pia walishiriki katika kazi ya Ablamu hiyo.

Alade amesema kuwa baadhi ya wasanii wanadai kutaka kutoa heshima kwa asili yao lakini ”wote wanaongea na hakuna kiteno”. Hii sio ukweli wa Beyoncé, aliiambia BBC.

“Kwa mtu wa hadhi yake kutoa muda wake na juhudi zake kwa Afrika , inaonyesha thamani yetu ,” aliongeza.

Afrobeats huenda ni aina ya muziki unaotamba zaidi nje ya bara la Afrika – na hususan nchini Uingereza. sambamba na Afropop na Afrofusion, sauti hizi zinatamba kwenye mawimbi ya vyombo vya muziki huku ikiwa juu kwenye orodha ya muziki inayopendwa na kwenye kumbi za densi kote duniani.

Albamu mpya ya Beyoncé’ ni jaribio linalosaidia kuchanganya ” Afrobeats halisi , pop halisi na sauti za R&B ” kwa ajili ya wasikilizaji wasio Waafrika , amesema mtangazaji wa Nigeria Adesope Olajide, al maarufu Shopsydoo.

Anasema kuwa muziki huu utapatikana kwa urahisi na ”niwa kuvutia zaidi” kwa msikilizaji wa aina hiyo.

“Hatimae unakuwa sauti ambayo sio Afrobeats asilia bali zinakuwa ni sauti bora ambayo yule msikilizaji wa Beyoncé ataweza kuisikiliza na kuielewa ,” Shopsydoo ameiambia BBC.

“Nafahamu mengi kuhusu mambo ambayo watu wanafikiria : ‘Labda atatuibia sauti na kutengeneza sauti yake’ lakini siamini hilo . Anawahusisha hawa vijana na wasichana , akishirikisha raha yake kwa misingi yao .”

  • Beyonce na Jay-Z watoa albamu pamoja, wamtaja Trump
  • Mwanamuziki Wizkid kutoka Nigeria atumbuiza Nairobi

Lakini si kila mtu anahisi hivyo.

Wakati Albamu ilipotolewa, wengi miongoni mwa wasanii wa Afrika mashariki walielezea kukatishwa tamaa kwa kuachwa nje ya kazi ya Beyonce. Wengi miongoni mwa wahusika wa filamu, wana majina ya kiswahili na vibonzo vya filamu halisia ya mwaka 1994 inaaminiwa kuwa ilichukuliwa nkatika eneo la Bonde la ufa nchini Kenya.

” Hatukuwakilishwa katika barua ya upendo kwetu . Inaumiza,” Mwanamuziki wa kenya Victoria Kimani alisema kwenye ukurasa wa Twitter.

Watu waliofanya vizuri zaidi hushirikishwa kwanza

Kabla ya to kuonekana katika albamu ya hivi karibuni ya Beyonce , baadi ya wasaniii hawa walikuwa tayari wanafanya vemakatika njia yao ya kutambuliwa duniani.

Muziki wa Wizkid uliingia nchini Marekani tangu 2016, wakati aliposhirikiana na mwanamuziki wa mtindo wa rap wa MCanada Drake katika wimbo wake uliotikisa mawimbi ujulikana kama One Dance, ambapo alikuwa Mnigeria wa kwanza kuingia katika chati ya miziki bora zaidi 100 na wimbo wake ukawa wa kwanza kuchezwa mara bilioni moja katika streaming service Spotify.

Mwaka huu pia Wizkid na Burn Boy walifanya onyesho katika Coachella nchini Marekani – moja ya moja ya matamasha makubwa zaidi duniani.

  • Watoto wa Nigeria waliomvutia Rihanna

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Burna Boy katika jukwa la Coachella mwezi April

Wakati huo huo Tiwa Savage, ambaye tayari alikuwa ana mkataba wa usimamizi na Jay-Z’s Roc Nation, alisaini mkataba wa kimataifa wa kurekodi miziki na Universal Music group mwezi Mei.

MNigeria mwenzake Tekno alisaini mkataba wa usambazaji wa muziki mwaka jana na Universal Music Group Nigeria na Island Records, na Yemi Alade amekuwa akifanya matamasha katika maeneo mbali mbali ya bara la Ulaya.

Kuonekana kwenye nyanja za kimataifa ni faida kwa nyota wa kimataifa na wasanii wa Afrika anasema mkurugenzi wa masoko ya kidigitali Kareem Mobolaji.

  • Nyota wa Afrika waliojumuishwa kwenye albamu ya Beyonce

“Wamarekani na wengine kwa sasa wameamka . Watu kama Wizkid wameonyesha namna uwepo wa nyimbo zao mtandaoni unavyoweza kusaidia kuongeza mauzo na kusikilizwa kote barani Afrika na kote duniani .”

Haki miliki ya picha
Kevin Mazur/Getty Images

Image caption

Wizkid alikuw ani msanii wa kwanza wa Nigeria kuuza tiketi zake zote za tamasha katika London’s Royal Albert Hall

Beyoncé pia atanufaika kwa kufanya kazi na wasanii nyota wa Afrika.

” Ni jukwa kubwa kwa mwanamuziki huyo wa pop na dunia nzima la kuwatambua wasanii wa Afrika “, na pia kupata “ufuasi mpya kwa ajili ya Beyoncé kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki maarufu wa pop barani Afrika “, alisema.

“Wafanyabiashara wenye ufanisi ni wale wanaoweza kufanya Kolabo kwanza .”

Kutambuliwa katika muziki

“Afrobeats na Afropop bila shaka ni aina ya muziki unaokuwa kwa kazi miongoni mwa watu weusi duniani baada ya hip-hop,” ameiambia BBC sema mtangazaji Shopsydoo.

“Hii ndio sababu inayowafanya wanamuziki nyota wa African pop kurekodi miziki yao katika nembo za rekodi za kimataifa .”

Kampuni ya usambazaji wa muziki kwa njia ya kidigitali TuneCore ilisema kuwa muziki wa dunia , katika kiwango ambacho zaidi muziki wa kiafrika unawekwa ni kile kicha muziki unaokua kwa kasi zaidi kw akiwango cha ongezeko la 57% mwaka 2018.

Mtiririko wa Music barani Afrika Africa pia umeshuhudia ukuaji wa 146% – ukiwa ndio unaokuwa kwa kasi zaidi duniani

Haki miliki ya picha
Lorne Thomson/Getty Images

Image caption

Tiwa Savage alisaini “hatua ya mamlaka ” ya mkataba wa kurekodi duniani na Universal Music Group mwezi May

“Muziki huu uliomuhusisha [Beyoncé feature] utavutia zaidi nembo za muziki za kigeni katika muziki wetu na kusaini mikataba zaidi na wasanii wetu ,”anasema Kareem Mobolaji, wa kampuni ya masoko ya kimtandao – Inglemind Concept Digital.

Kampuni ya kimataifa ya kurekodi muziki kama vile Universal Music Group imekwishapanuka zaidi katika bara ikiwa na ofisi zake katika mataifa ya Nigeria, Kenya, Ivory Coast na Afrika Kusini.

Wakati huo huo Sony Music, ina ofisi zake Nigeria na Afrika Kusini . Warner Music Group, a,mbayo iko tayari nchini Afrika Kusini , pia hivi karibuni ilisaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya kurekodi muziki ya Nigerian -Chocolate City.

Uhusiano wa Beyoncé na Waafrika

Mashabiki wa mwanamuziki wa Marekani Beyoncé wamekuwa wakishirikisha kipande cha video cha mwaka 2009 ambapo muimbaji huyo alifichua jukwaani kuwa mababu zake walikuwa ni Wanaigeria , kabla ya kuimba wimbo wa taifa hilo:

Mapenzi ya Beyoncé kwa bara la Afrika yamekuwa yakidhihirika kwa miaka kadhaa kupitia picha zake , video zake za muziki na maneno , matamasha yake na hata chaguo lake la mitindo ya mavazi. maperformances and fashion choices.

Mara kwa mara amekuwa akiwaunga mkono wanamitindo wa Kiafrika – alionyesha kazi ya wanamitindo wa Afrika Kusini Afrikanista na MmusoMaxwel mjini Johannesburg mwaka jana , na Msenegali Sarah Diouf hivi karibuni.

Msanii wa picha Laolu Senbanjo, anayejulikana kwa usanii wake wa picha wa Sacred Art of the Ori, aliwavalisha Beyonce na wanenguaji wake kwa mchoro wa mwili kwa ajili ya video yake ya muziki ya mwaka 2016 ijulikanayo kama Sorry.

Beyoncé pia alijifananisha na miungu ya Yoruba Oshun, muungu wa kike mwenye uwezo wa kuzaa na Mungu wa kike Yemoja, wa maji , katika tamasha la tuzo ya Grammy la mwaka 2017 na picha yake ya chini ya maji alipokuwa mjamzito

Haki miliki ya picha
Kevork Djansezian/Getty Images

Image caption

Beyoncé alitumia picha ya kufikirika ya Oshun wakati wa tamasha la tuzo ya Garammy ya mwaka 2017

Wasanii walioshiriki katika Albamu ya The Lion King: The Gift wanasema uungaji mkono wa Beyoncé’s wa kipaji chao unaonyesha kile hadhira ya Waafrika ilichokifahamu kwa muda mrefu.

“Ninahisi kana kwamba huu ni muda mzuri na mengi yatakuja ,” Yemi Alade aliiambia BBC.

Shabiki mkubwa wa Beyoncé wa Afrika Kusini Moonchild Sanelly, abaye amekuwa na ndoto ya kushuhudia colabo hiyo ,anaafikiana na Alade

“Sasa hivi nimekwisha weka alama ya ndio kwenye boksi la wakati wa maisha yangu na kwanza ndio nimeanza.”Source link