Rapper Chris Brown ameoneshwa kukerwa na mavazi ya mchumba mpya wa aliyekuwa Girlfriend wake, Karrueche Tran aitwaye Victor Cruz kwa kudai kuwa mwanaume huyo hajui kuvaa.

Chris Brown ametoa maoni hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ambapo amemshauri mrembo Karrueche kumpeleka kwake ili amfundishe kuvaa vizuri.

Tukio hilo, limejiri wiki iliyopita baada ya Karrueche kuposti picha akiwa na Boyfriend wake kisha Chris Brown akaanza kutoa maneno hayo kwenye kisanduku cha maoni.

Wiki iliyopita ilikuwa ni wiki ya wanaume kupendeza, hivyo Karrueche na mpenzi wake huyo waliposti picha kwenye mitandao ya kijamii ambazo zilikuwa zinawaonesha wakiwa mitaani mjini Miami.

Kwenye maoni hayo yamesomeka “Sio kwamba ni wivu, Ila jitahidi kumvalisha. Anaonekana kama nguo zilizowekwa kwenye kinyago na mnunuzi anataka kupunguziwa bei,”.

Chris Brown alishawahi kuwa kwenye mahusiano na Karrueche na tangu waachane Chris amekuwa akimfuatilia kwa ukaribu kwenye mitandao ya kijamii.Source link