Jose Mourinho amefunguka kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumpigia simu mara baada ya kupata kazi ndani ya klabu ya Tottenham alikuwa Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Manchester United, Ed Woodward.

Mourinho believes his relationship with new boss Daniel Levy will be strong going forward

Mreno huyo alitimuliwa kazi na Woodward miezi 11 iliyopita kutokana na Manchester United kusuasua kwenye michezo yake.

Inaonekana historia yao haijaathiri uhusiano wao ingawa na Mourinho akitanabaisha kuwa Woodward alikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kumpigia simu baada ya kuthibitishwa kama kocha mpya wa Spurs akichukua mikoba ya Mauricio Pochettino.

Mourinho na Ed Woodward

Mourinho aliwaambia Sky Sports, ”Pengine nimepata nafasi ya kuomba radhi kwa kushindwa kupokea zaidi ya simu 500 nilizopigiwa na kushindwa kujibu. Kwa sasa nina 700 lakini nimejibu 200 tu.

”Lakini zilikuwa za matumaini, kutoka kwa klabu yangu ya mwisho. Hivyo watu wengi wamenionyesha heshima, huruma na hisia zao ni vizuri.”

”Wote walikuwa maalum, wakwanza kabisa alikuwa Mkurugenzi wa United, Richard Arnold, watatu, wanne au watano alikuwa Ed Woodward. Na alikuwa bosi wangu.” Amesema Mourinho.

Mourinho anaamini mahusiano yake na bosi wake mpya, Daniel Levy yatakuwa zaidi ni ya kijamii ”Nafikiri tutaendelea vizuri. Ameniambia mipango ya klabu na kuele inapohitaji kufika nikakubaliana na hilo. Na hilo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya mimikukubali.”Source link