Klabu ya Simba kutoka Tanzania imetolewa kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Afrika kwa kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya UD Songo ya nchini Msumbiji.

Goli la kusawazisha la Simba SC, Limefungwa na Erasto Nyoni huku la UD sonko likifungwa na Luis kunako dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza cha mchezo.

Mchezo wa kwanza Simba SC walitoka Srae ya 0-0 dhidi ya UD Sonko, Hivyo kwa matokeo hayo UD Sonko wanasonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.

Simba SC inakuwa ni timu ya pili kutoka Tanzania kutolewa kwenye michuano kimataifa ya CAF, Baada ya klabu ya KMC FC ya Kinondoni kutolewa Ijumaa hii kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.Source link