Baada ya kupoteza fainali ya MapinduziCup – Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya #SimbaSC, Mohammed Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi yake na kubaki kama Mwekezaji.

Mo ameandika ujumbe huo dakika chache tu baada ya @simbasctanzania kupokea kichapo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Mtibwa Sugar na kupelekea kukosa Ubingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi

Vijana wa Mtibwa Sukari walipata bao la mapema kunako dakika ya 38, kupitia kwa Awadhi Salum Juma ambalo limepelekea kudumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Simba SC na Mtibwa Sugar zote zilikuwa kundi B katika michuano hii group ambalo ndiyo limetoa be bingwa. Wakati Bingwa wa kombe la Mapinduzi 2010 @mtibwaofficial wakiwasukumiza nje ya michuano hii #yangasc kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya  dakika 90′ kumalizika  1-1 huku @simbasctanzania wakiwatoa Mabingwa watetezi @azamfcofficial hatua ya nusu fainaliSource link