Floyd Mayweather anasema 2020 anarudi katika ulingo wa masumbwi ama ndondi. Kupitia mtandao wa Instagram Mayweather Jr ametangaza nia yake ya kusitisha kuwa mstaafu.

Ikumbukwe hii sio mara ya kwanza kwa Floyd Mayweather kutangaza kustaafu kisha baadae kurudi ulingoni. Alitangaza kustaafu tangu mwaka 2007 baada ya kumchapa bondia Ricky Hatton, alirudi ulingoni mwaka 2009 mpaka 2015 ambapo alitangaza tena kustaafu baada yakuchapana na Manny Pacquiao.

Lakini haikuishia hapo mabondia wengine waliendelea kumtaka ulingoni wakitaka kulipa kisasi wakiwemo Connor na Alvarez.


Floyd alirejea tena mwaka 2017 ambapo pia alimtandika Conor McGregory huko Nevada na kukamilisha mapambano 50 ya ushindi. Sasa ana miaka 42 akiwa na mapambano rasmi 50 na kushinda yote.

By Ally Juma.

Source link