Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Haji Manara amesema yupo tayari kuwajibishwa kufuatia timu yake kutupwa nje ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Manara amesema kwanza anaomba radhi kwa mashabiki wa Simba SC, Na kudai kuwa matokeo hayo ni fedheha kubwa klabu hiyo.

‚ÄúAm Sorry Guys ūüôŹ Hakika huu ni msiba na ni fedheha kuu. Nipo tayari kuwajibika kwa matokeo haya, Nawaomba tena Samahani Washabiki wetu.‚Äúameandika Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, Mwenye kubeba jukumu la kiufundi ndani ya kalbu ni Kocha Mkuu na Benchi la ufundi na sio jukumu la msemaji wa klabu kama yeye anavyotaka kuwajibishwa.

Leo Klabu ya Simba imetupwa nje ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika, Kwa kutoka sare ya 1-1 na klabu ya UD Songo kutoka Msumbiji.

Soma zaidi : http://bongo5.com/breaking-simba-sc-watupwa-nje-michuano-ya-klabu-bingwa-afrika-yaungana-na-vijana-wa-kinondoni-kmc-08-2019/

 Source link