Mwanasheria Mkuu wa wa Israel, Avichai Mandelblit amemfungulia mashtaka ya kupokea hongo, udanganyifu na kuvunja uaminifu, Benjamin Netanyahu.

Avichai Mandelblit (kushoto) na Benjamin Netanyahu (kulia)

Waziri huyo Mkuu wa Israel, Netanyahu ameyakanusha madai ya ufisadi dhidi yake na amesema ataendelea na majukumu yake kama kiongozi licha ya kufunguliwa mashtaka ya rushwa.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Deutsche Welle, Benjamin Netanyahu aliishutumu hatua hiyo na kuyataja kuwa uongo na njama za kisiasa. Aidha ameitaja hatua hiyo kama jaribio la mapinduzi dhidi ya waziri mkuu.

Image result for Avichai Mandelblit

Benjamin Netanyahu

Hatua ya kumfungulia Netanyahu mashitaka imejiri wakati Israel ikikumbwa na mparaganyiko wa kisiasa na inakabiliwa na uwezekano wa kufanyika uchaguzi kwa mara ya tatu ndani ya mwaka mmoja, baada ya Netanyahu na hata aliyekuwa mshindani wake Benny Gantz kushindwa kuunda serikali.Source link