Kevin OdourHaki miliki ya picha
Kevin Odour

Image caption

Kevin Odour

Kevin odour mwenye umri wa miaka 24, alizaliwa na virusi vya ukimwi na sasa ameweza kupata mtoto asiye na virusi hivyo.

Kevin amesema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Afya cha BBC juu ya safari yake ndefu inayostaajabisha na kusisimua lakini jambo kubwa anajivunia maisha yake.

  • Sababu inayopelekea ngono salama kuepukwa?
  • Kondomu zazua hofu Tanzania

”Safari yangu ya kuishi na virusi ilianza nilipozaliwa lakini nilianza kumeza dawa za virusi nikiwa na umri wa miaka sita wakati ambapo nilianza kuugua mara kwa mara na kulazwa hospitalini,” Kevin alieleza.

Aliongeza kusema kuwa wakati alipoanza kulazwa mara kwa mara hospitalini na kumeza dawa za kifua kikuu alikuwa hafahamu kama ameathirika.

Image caption

Dawa za virusi vya ukimwi

“Baada ya kufanyiwa uchunguzi walinipatia dawa lakini hawakuniambia zilikuwa ni za nini na hata mama yangu pia hakuniambia lakini kila siku nilikuwa nikijuuliza hizi dawa ni za nini na kwa nini nakunywa kila siku?

Nilipofika darasa la sita nikamuuliza mama yangu; mbona dada yangu hamezi hizi dawa lakini ni mimi na wewe tu?

Akaniambia kwamba muda ukifika ataniambia , alisisitiza kwamba nikiendelea kukua atanieleza lakini na nikaendelea kumeza dawa hizo huku nikiendelea na masomo yangu.

Nilipofika umri wa miaka tisa niliamua kutomeza dawa hizo na hapo ndipo nilipoanza kuugua sana.

Image caption

Virusi vya ukimwi

Baadae niliamia katika nyumba ya watoto wadogo waliozaliwa na virusi vya Ukimwi na wale wasio na wazazi.

Huku ndipo nilikutana na watoto wengine kama mimi wakimeza dawa nilizokuwa nikimeza hapo awali lakini swali la kwa nini ninameza dawa hizi bado lilikuwa akilini mwangu.

Maswali haya yote yalifika kikomo pale ambapo mtawa mmoja alipotutembelea katika nakazi yetu na akiongozana na nesi mmoja na kutuuliza iwapo tunafahamu kuhusu hali zetu?

  • ‘Sugar mummy’ aliniponza nikapata virusi vya Ukimwi

Nilijiangalia na nikajiuliza ni hali gani hiyo? Basi nesi huyo hakuficha akatuuliza iwapo tunafahamu kama tuna virusi vya ukimwi?

Habari hiyo ilinishtua sana nakujiuliza kuwa hizi dawa ambazo nimekuwa ninameza kila siku ni za Ukimwi.

Kwa familia yetu mimi peke yangu ndio nilikuwa nimezaliwa na virusi hivyo vya Ukimwi.

Baada ya kusikia hayo ikawa ni mara ya pili ninaapa kuwa “sitakunywa tena dawa hizo”.

Lakini baada ya kupata taarifa hiyo ambayo ilinishtua nikaamua kumuuliza mama yangu iwapo yeye pia ana virusi vya ukimwi?

Alishtuka lakini akakiri kwamba ana virusi vya ukimwi na hiyo ndio siku aliamua kufunguka kuniiambia kuhusu hali yake na yangu.

Niliweza kubaini kuwa mama yangu ana saratani lakini vilevile anaishi na virusi vya Ukimwi.

Kisa hicho cha mama yangu kilinifanya nimuhakikishie kuwa sitaacha tena kumeza dawa, nitaishi na kujenga familia.

Nilipitia unyanyapaa nilipokuwa nakua , marafiki zangu walikataa hata kucheza mpira na mimi wakidhani kuwa nitawaambukiza.

Wengine waliogopa kucheza na mimi kwa hofu ya kuambukizwa na taratibu nikajitenga nao.

Haki miliki ya picha
Kevin Odour

Image caption

Kevin Odour

Ndoto yangu ilikuwa ni kuwa na familia, nilikutana na msichana ambaye nilimpenda ingawa ilinichukua muda kumwambia kutokana na hali yangu.

Sikuwa na matumaini kuwa atanikubali kama nikimwambia hali yangu lakini cha kushangaza alinikubali huku akijua hali yangu ya kiafya.

Mke wangu hakuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi mpaka sasa hana virusi hivyo.

Miaka saba iliyopita ndipo nilimwambia kuhusu hali yangu mbele ya daktari na akanihakikishia ataiishi nami na alimshukuru kwa kumwambia mapema.

Na tangu hiyo siku nilimuahidi kutomuacha maishani kwangu.

Baada ya miaka kadhaa mke wangu alipata uja uzito na kujifungua mtoto msichana ambaye hana virusi vya ukimwi pia,” Kevin alisimulia.

Kulingana na wataalam mtoto anastahili kufahamisha hali yake akiwa kati ya umri wa miaka 6 hadi 9.Source link