watoto waomba barabaraniHaki miliki ya picha
AFP Contributor

Yoyote anayewapa pesa chakula au msaada watoto wanao ombaomba katika mji mkuu wa Uganda, Kampala wanaweza kufungwa mizi 6 gerezani.

Hii ni baada ya sheria mpya kupitishwa leo iliyonuiwa kusitisha watoto kutimiwa vibaya.

Ni picha iliyozoeleka unapokuwa katika mitaaya Kampala: watoto walio na umri wa chini kama miaka 7 hivi wakizunguka na kujipenyeza katikati ya magaari wakati wa foleni wakiuza biadhaa au wakiomba.

Lakini sasa ni kinyume cha sheri aiwapo mtu atamsaidia mtoto anayeomba kwa kumpatia pesa au achakula na hukumu yake ni kuishia gerezani kwa miezi sita au utozwe faini ya $11.

Meya wa mji wa Kampala, Erias Lukwago, amesema sheria hiyo pia itawahukumu wasafirishaji haramu wa watoto, maajeni na wazazi wa watoto watakaokutikana wakiomba au wakiuza vitu barabarani.

Serikali inakadiria kuwa kuna watoto wanaozidi 15,000 walio na umri wa kati ya miaka 7 na 17 omitaani na idadi hiyo inaendelea kuongezeka.

Baadhi ya watoto hao husafirishwa kiharamu kutoka vijijini na hukodishiwa vyumba katika mitaa ya mabanda na wasimamizi wao.

Sheria pia inapinga mtoto kukodishiwa nyumba ili kushiriki vitendo vya utovu nidhamu au kwa mtoto kujishughulisha na biashara ndodo.

Kumekuwa na wasiwasi kwamba baadhiya watu huwatumia watoto wadogo kupata pesa kupitia njia hiyo ya kuomba omba barabarani.

Haki miliki ya picha
AFP

Hili ni tatizo la sio tu Kampala wakati katika baadhi ya miji mikubwa katika mataifa ya Afrika, watoto huonekana kuyavizia magari wakati wa foleni kubwa barabarani na kuomba msaada.

Watoto hao huonekana mjini wakati kunapokuwa na shughuli nyingi na msongamano wa magari ima ni asubuhi wakati watu wanakwenda kazini au hata jioni wakati watu wanapotoka kazini kurudi nyumbani.

Nchini Kenya kwa mfano maafisa wa baraza la mji na mitaa mara kadhaa wameidhnisha misako kuwafukuza watoto wanaoomba barabarani na mara nyingine kuwapeleka katika makao maalum.

Lakini hilo halijasaidia.

Mara kwa mara operesheni kama hizo zimekuwa zikiidhinishwa katika jitihada za kukabiliana na kuongezeka kwa visa vya uhalifu.

Kulikuwa na malalamiko ya kuongezeka visa vya watoto wa kuomba mitaani wanaowashambulia wakaazi na kuwaibia au hata mara nyingine kuwanynyasa kingono wapita njia.

Licha ya kwamba katika operesheni hizo watoto hao hukusanywa na kuepelekwa katikamakao maalum, muda sio muda wao hurudi tena barabarani.

Inasubiriwa kuonekana iwapo sheria hii mpya Uganda itasaidia katika kuwaondosha watoto wanaoomba Kampala na kupunguza uhalifu unaoshuuhdiwa.

Baadhi ya watoto wanao omba mitaani inaarifiwa pia hulazimika kuja katika miji mikuu kama Kampala kuomba kutokana na kukithiri umasikini.Source link