Wiki iliyopita Shirika la habari nchini Uingereza Sky News lilionesha sura ya mtu aliyeingia kwa kujificha kwenye ndege moja inayomilikiwa na shirika la ndege la Kenya Airways, wakati ikijitaharisha kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London, mwezi Juni.

Ripoti iliyotolewa na mwandishi wa habari kutoka Afrika John Sparks, ilimtaja mtu huyo kuwa ni mfanyakazi wa uwanja wa ndege mjini Nairobi alifahamika kama Paul Manyasi.

Hii ilitokana na mahojiano na watu ambao walijitambulisha kama marafiki, ndugu na wafanyakazi wa Paul Manyasi akiwemo baba yake mzazi.

Katika mahojiano na gazeti moja nchini Kenya, mwanaume huyo amekiri kuwapotosha chombo hicho cha habari, Sky News.

Kulingana na habari kutoka gazeti la Daily Nation, mtoto wake aliyetajwa kwenye ripoti hiyo kama Shivonje Isaac yupo hai ndani ya rumande katika gereza moja nchini Kenya.

Sky News imesema inajutia kuwa ripoti yake iliandaliwa kwa kutumia maelezo yanayopotosha .

Shirika la Ndege nchini Kenya lilikiri kuwa hapo awali inawezekana kuwa mtu huyo aliyejificha alikuwa ni mfanyakazi ndani ya uwanja huo wa ndege mjini Nairobi.

Lakini hatuna ushahidi wa kutosha kusema kwamba mtu huyo alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya kufanya usafi ya Colnet, hivyo basi tunaomba msamaha kwa kampuni ya Colnet kwa kudhania mtu huyo alikuwa mmoja wa wafanyakazi wake.

MkobaMkoba huu ulipatikana kwenye gia ya kutua ya ndege ambako mwanaume alikuwa alipodondoka kutoka kwenye ndege

Tukio hilo lilikuwaje?

Mamlaka za gereza ziliiambia BBC kuwa mwanaume huyo ambaye alioneshwa kwenye picha ni Cedric Shivonje Isaac ambaye amekuwa akizuiliwa tangu mwezi Agosti, na si Paul Manyasi, ambaye alitambuliwa katika taarifa ya Sky News.

Uchunguzi wa shirika la habari Sky News wiki hii ulionekana kuthibitisha sura ya mtu huyo. Ripoti ilionesha sura ya mwanaume ambaye Sky News iliambiwa kuwa alifanya kazi kwenye kampuni ya usafi kwenye uwanja wa ndege, na ambaye anadaiwa kujificha kwenye eneo la chini ya gia ya ndege.

Lakini sasa imebaini kuwa mwanaume aliyeonekana kwenye picha hizo yuko hai na amekuwa akishikiliwa na polisi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Mamlaka za gereza zimethibitisha kuwa jina la mwanaume huyo ambaye alionekana kwenye picha kwenye ripoti ya Sky News ni Cedric Shivonje Isaac. Baba wa mwanaume huyo amekana kauli yake alipozungumza na mtangazaji , na sasa anasisitiza mtoto wake bado yu hai.

Haijajulikana mkanganyiko huu umetokea vipi, wapelelezi wanajaribu kutafuta uwezekano kati ya bwana Isaac, mtu aliye kwenye picha na bwana Manyasi, mwanaume aliyetambuliwa kwenye ripoti.

Taarifa hii imezua maswali mapya kuhusu uwezo wa mamlaka za Kenya kumbaini mtu aliyeingia ndani ya ndege hiyo, ikiwa miezi minne tangu alipoanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London.

https://www.nation.co.ke/news/Sky-New-stowaway-reporting-misleading-information/1056-5357234-dysj4e/index.html

By Ally Juma.Source link