Rais wa klabu ya Sporting Lisbon kutoka nchini Ureno amethibitisha kuwa  anataka kubadili jina la uwanja wake Estadio Jose Alvalade wenye uwezo wa kubeba mashabiki 50,000 na kuupa jina la nyota wa klabu ya Juventus na taifa la Ureno Cristiano Ronaldo na kuitwa “Cristiano Ronaldo Arena au CR7 Arena”

Ikumbukwe uwanja wa nyumbani wa Sporting Estadio Jose Alvalade, ulipewa jina la mwanzilishi wa klabu hiyo Jose Alvalade mwaka 1956 lakini ripoti zinasema Sporting inafikiri kubadili jina na kuupa jina la mchezaji waliyemlea katika Academy yao na na baadaye kucheza katika kikosi cha kwanza kabla hajaondoka kwenda Manchester United (2003).Sasa ni miaka 17 tangu Ronaldo atengeneze jina katika taaluma ya Sporting. Alianza kazi yake na kilabu ya Sporting na nyuma msimu wa 2002-2003, Ronaldo akawa mchezaji wao wa kwanza kucheza kwenye timu ya chini ya miaka 16, timu za chini ya miaka 17 na chini ya 18, timu ya B, na timu ya kwanza, yote ndani ya msimu mmoja.

“Ni nadharia ambayo hatutaiweka kando na ni wazi tumekuwa tunajivunia sana kuwa na jina lake kuhusishwa na sisi. Cristiano yuko na kila wakati atakuwa alama kubwa katika historia ya kilabu yetu,” Rais wa Sport Frederico Varandas aliiambia Tuttosport.

Alizidi kusema kuwa “Ni urithi wa Ronaldo unaochochea kizazi kijacho kwenye kilabu hii. “Tayari tunatunza maadili yake kwenye ukuta wa uwanja wa vijana,youth academy, tukizingatia shauku, kujitolea, nidhamu, uongozi na uamuzi.

“Cristiano hakika ni mchezaji bora wa Ureno wa wakati wote na mmoja wa wachezaji bora katika historia ya mchezo huu wa mpira wa miguu,” Varandas aliongeza.

By Ally Juma.Source link