Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Sven Vanderbroeck ametaja malengo yake na kile kilichomvutia ndani ya timu hiyo, ambayo anarithi mikoba ya Patric Aussems aliyetimuliwa kazi hivi karibuni.

Vanderbroeck amesema malengo yake ya kwanza ni kuhakikisha anachukua ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

“Lengo la kwanza ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu. Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, nataka kucheza mashindano ya CAF. Nataka Simba iwe kwenye hatua kubwa na kupata matokeo mazuri,” Amesema Vanderbroeck.

Sven Vanderbroeck ameongeza kuwa “Kilichonivutia Simba cha kwanza ni uwingi wa mashabiki. Ni jambo la kufurahisha kuona mashabiki 60,000 wakikushangilia inakupa hisia za kipekee”- Kocha Mkuu mpya, Sven Vanderbroeck.

Sven Vanderbroeck ametangazwa rasmi na miamba hiyo ya soka ya Tanzania Bara hapo juzi siku ya Jmatano ya tarehe 11/ 12/ 2019 ambapo alichukua nafasi ya Aussems ambaye aliifundisha Simba SC kwa mafanikio makubwa akiiwezesha kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu bingwa Barani Afrika kwa mara ya kwanza, akiutetea ubingwa wa ligi na kuuchukua msimu wa mwaka 2018/19 huku ikiweka timu hiyo katika nafasi nzuri kwenye ramani ya soka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla baada ya Wekundu hao wa msimbazi kupanda kwenye viwango vya soka Afrika na hata kuwezesha Tanzania kupeleka timu nne kwenye michuano mikubwa Afrika kombe la Shirikisho na Klabu bingwa.

Source link