Kim Jong-un na Donald Trump wakisalimianaHaki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Kim Jong-un na Donald Trump wakati wa furaha 2018

Korea Kaskazini imeimarisha matusi yake dhidi ya rais Donald Trump baada ya kutishia kuchukua hatua za kijeshi .

Waziri wa maswala ya kigeni amesema kwamba rais Trump ni mchokozi na kwamba anafaa kuchunguzwa akili.

Korea Kaskazini kwa mara ya kwanza ilimuita rais Trump kuwa ‘mzee aliyedhoofika kiakili 2017’.

Ni mara ya kwanza baada ya kipindi cha mwaka mmoja kwamba Pyongyang imekuwa ikimkosoa Donald Trump waziwazi kulingana na mwandishi wa BBC Laura Bicker.

Kamusi ya Oxford inaelezea neno ‘Dotard’ kama mtu ambaye akili yake imedhoofika hususan mzee ambaye uelewa wake umedhoofika .

‘Dotage’ inaelezewa kuwa kutokuwa na uelewa katika miaka ya uzeeni ama kwa matumizi ya jumla kama umri wa uzeeni.

Wawili hao walifanya mazungumzo ya ana kwa ana nchini Singapore mnamo mwezi Juni 2018 na Vietnam mnamo mwezi Februari mwaka huu yanayolenga kusitisha mipango ya kinyuklia ya taifa hilo.

Lakini mazungumzo yamekwama tangu wakati huo, na licha ya mkutano mwengine kufanyika katika eneo la mpakani linalozigawanya Korea Kaskazini na Korea Kusini mwezi Juni, upande wa Kaskazini ulianza tena kufanyia majaribio makombora ya masafa mafupi.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Korea kaskazini imefanyia makombora yake majaribio katika kipindi chote cha mwaka 2019

Katika miezi ya hivi karibuni maneno hayo machafu yametumika tena

Pyongyang imeipatia Washington makataa ya mwisho kuipatia mapendekezo yake ya mwisho wa mwaka kuhusu mipango yake ya kinyuklia na imesema kuwa itatoa mwelekeo mpya iwapo hilo halitafanyika .

‘Vita vya maneno’

Katika mkutano wa Nato nchini Uingereza siku ya Jumanne , bwana Trump alimtaja kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kama ‘rocket man’.

Aliongezea kwamba Marekani ina kila uwezo wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Pyongyang.

Katika taarifa iliotolewa na chombo cha habari cha Korea Kaskazini , makamu wa rais Choe Son Hui alionya kwamba vita vya maneno vilivyoanza miaka mwili iliiopita huenda vikaanza upya.

Iwapo lugha yoyote ama maneno yanayoweza kuchafua mazingira yaliopo yatatumika kwa lengo fulani na katika wakati muhimu, hiyo itachukuliwa kama ‘akili ya mtu mzee iliodhoofika’.

Mwaka 2017, viongozi hao wawili walikabiliana kimaneno huku rais Trump akimuita bwana Kim kama mtu mdogo “little rocket man” na mwendawazimu huku naye bwana Kim akimuita rais huyo wa Marekani mtu ambaye akili yake ni punguani.Source link