Kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers ameongeza kandarasi ya miaka mitano na nusu ndani ya timu ambapo atasalia hapo mpaka mwaka 2025 na hivyo kuvunja kabisa uwezekano wa kutua Arsenal kama ilivyotarajiwa na waliyowengi.

Image result for brendan rodgers

Rodgers ambaye amewahi kuifundisha Liverpool na Celtic alikuwa kwenye orodha ya makocha ambao walikuwa wakiwindwa na Arsenal baada ya kumtimua kazi Unai Emery wiki iliyopita.

Hata hivyo kwa upande wake amesema kuwa amekuwa mwenye furaha kubwa ndani ya Leicester ambayo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Premier League.

Leicester City imekuwa na mafanikio ya ghafla kwenye ligi kuu England, ambayo imepelekea kushika nafasi ya pili hivyo kuzua utata kwa baadhi ya klabu kutamani kumng’oa kocha wa timu hiyo, Brendan Rodgers hali iliyopelekea Mbweha hao kuhakikisha wanambakiza,  ili kuvuna walichopanda.

Rodgers mkataba wake ulikuwa unaisha mwaka 2022, lakini baada ya kuanza tetesi za kuondoka King Power Stadium ndipo Leicester City ikaamua kumuongezea mkataba.

 Source link