Woman and children at outpost of Migron (file photo)Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mamia ya waisraeli wanaishi katika makazi ya wayahudi katika ukingo wa magharibi

Makazi ya wayahudi katika eneo la wapalestina katika ukingo wa magharibi na mashariki ya Yerusalemu ndio yamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro kati ya Israel na Palestina.

Kwa jumuiya za kimataifa, ni kinyume na sheria Israel kuwapeleka raia wake wengi katika ardhi iliyoinyakua na kukalia wakati wa vita vya siku sita mwaka 1967.

Marekani ilikuwepo kwenye sehemu ya makubaliano ya kimataifa na ilikuwa inatambua kuwa makazi hayo yamechukuliwa kinyume na sheria lakini siku ya jumatatu 18, 2019 ilibadili uamuzi wake.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ametangaza kuwa serikali yake haitaendelea kutambua makazi ya wayaudi yaliopo ukingo wa magharibi kuwa hayapo kisheria.

Kusema kuwa makazi ya wayahudi ni haramu hakujasuluhisha lolote . Amani haiwezi kupatikana kwa njia hiyo,” Pompeo alisema.

  • Mataifa ya kiarabu yaionya Israel kuhusu ‘mipango yake ya unyakuzi’
  • Israel ni taifa la Wayahudi rasmi

Mamlaka za Palestina zinasema kuwa maeneo wanayoyamiliki wanataka kuwa sehemu ya taifa lao kwa siku zijazo.

Palestina imepinga maamuzi ya Marekani kwa kusema kuwa ni hatari kwa usalama wa kimataifa, na kusema kuwa inatishia kuondoa sheria za kimataifa na badala yake kutumia sheria mbaya.

Waziri mkuu wa Israel anasema kwamba mabadiliko hayo ya sera , yanahalalisha makosa ya kihistoria na kutoa wito kwa mataifa mengine kuchukua hatua kama hiyo.

Kulingana na mwandishi wa BBC katika eneo la mashariki ya kati Barbara Plett-Usher, hatua hiyo itakandamiza mchakato wa kuafikia amani kati ya mataifa hayo mawili.

Tunaangazia masuala muhimu kusaidia kuelewa mzozo kati ya Israel – Palestina

Je makazi ya Israel ni yapi?

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Waziri mkuu wa Israel aliapa kutoyaamisha makazi ya wayahudi tena

Makazi hayo ya Wayahudi yalijengwa na Israel katika ardhi hiyo mwaka 1967 wakati wa vita vya mashariki ya kati.

Hii inashirikisha ukingo wa magharibi, Mashariki mwa Yerusalemu ambayo awali ilikuwa imekaliwa na Jordan , na milima ya Golan ambayo iliokuwa inamilikiwa na Syria.

Baadhi ya wakazi walienda katika eneo hilo kutokana na sababu za kidini , wakiamini kwamba Mungu aliwapatia wayahudi ardhi hiyo.

Wengine wamevutiwa na makazi hayo kwa kuwa nyumba katika eneo hilo ziko rahisi kulipa.

Makazi hayo yako wapi?

Kwa mujibu wa shirika la Israel linalopigania amani katika eneo hilo, kuna makazi 132 yaliojengwa bila ruhusa katika eneo la ukingo wa magharibi.

Kundi hilo linasema kwamba zaidi ya wakazi 413,000 wanaishi katika eneo hilo huku idadi hiyo ikiongezeka kila uchao.

Linasema kwamba kuna makazi 13 katika eneo la mashariki mwa Yerusalemu , yanayokaliwa na takriban watu 215,000.

Israel pia ilijenga makazi katika eneo la Gaza , na katika eneo la Sinai , iliyoichukua kutoka Misri mwaka 1967, lakini imeyaondoa makazi hayo.

Makumi ya makazi hayo yapo Golan , yaliyotolewa Syria katika vita vya mwaka 1967.

Makazi yaliyojengwa yamechukua asilimia mbili ya ukingo wa magharibi lakini eneo kubwa la ardhi hiyo ina shughuli za kibinadamu kama kilimo na barabara na kuna uhitaji wa jeshi.


Kwa nini makazi hayo ni chanzo cha migogoro?

Haki miliki ya picha
Getty Images

Kile kilichotokea katika makazi ya wayahudi ndio tatizo kubwa kati ya waisraeli na wapalestina na kusababisha kushindwa kupatikana kwa suluhisho la mazungumzo kadhaa ya amani.

Makazi ya wayahudi sio tatizo kwa wapalestina peke yake kwa sababu ardhi hiyo ilichukuliwa lakini pia uhuru wao ulikuwa umeminywa kwa kuepo kwa vizuizi vingi mpakani vya kuingia katika eneo hilo ambalo linalindwa na askari wa Israel.

Licha ya kuwepo kwa vizuizi vingi mpakani, wapalestina wanasema kuwa ukingo wa magharibi na mashariki mwa Yerusalemu , ni ardhi ambayo wanaitaka iingie kwenye taifa lao kwa siku zijazo na hicho ni kizuizi kwa Palestina.

Lakini pia wanataka Israel kuondoa shughuli zote wanazozifanya katika maeneo hayo kabla ya kukutana tena kwa ajili ya mazungumzo ya amani.

Israel inasema kuwa wapalestina wanatumia kigezo cha makazi ya wayahudi kuwa kigezo cha kukwepa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja nao.


Kipi kilichobadilika kwenye utawala wa rais wa Marekani Donald Trump?

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Rais Donald Trump amekosoa uamuzi wa Israel mara chache sana

Kwa maneno mawili, mengi yamebadilika.

Tangu rais Trump aingie madarakani mwezi Januari 2017, Trump amekuwa akionekana kuwa na mawazo tofauti dhidi ya makazi hayo tofauti na mtangulizi wake , Barack Obama.

Mpaka bwana Trump alipoingia madarakani, Marekani ilikuwa inatambua kuwa makazi hayo yapo kinyume na sheria ” – Ingawa haikuwahi kuyaita haramu tangu utawala wa ‘Carter’ mwaka 1980.

Idara ya usalama ya umoja wa mataifa ilikuja na mapendekezo mwezi desemba mwaka 2016 na kusema kuwa hakuna makazi yasiyotambulika na katiba haiwezi kukiukwa na sheria ya kimataifa.

Hata hivyo Israel pia ilieleza kuwa umoja wa mataifa haifungwi na sheria .

Tarehe 18, Novemba 2019, waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema kuwa utawala wa Trump unaenda tofauti msimamo wa utawala wake uliopita.

“Makazi ya raia wa Israel hayategemei sheria za kimataifa,” Bw. Pompeo alisema

Utawala wa Trump umebadilisha sera ya Marekani kwa kuutambua mji wa Yerusalemu na Golan kuwa sehemu ya Israel na kulinda makazi ya wayahudi.


Je makubaliano baina yao yanaweza kuwa jambo lisilowezekana?

Ni kama tatizo linaongezeka.

Kwa miaka mingi, Israel ilikuwa imejiandaa kutaka mambo magumu ili amani ipatikane ili iweze kutoa makazi yake katika eneo hilo kwa kuanza na kuondoa makazi madogo madogo

Awali Israeli iliyaondoa makazi ya Sinai na Gaza na makazi manne madogo yaliyoko ukingo wa magharibi mnamo mwaka 2005.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Israel iliyaondoa makazi ya Gaza 2005

Wakati Israel na Palestna walipoamua hatima ya makazi ya Yerusalemu katika mazungumzo ya mwisho ya amani, fursa za kufikia suluhisho la kudumu bado kuna safari ndefu.


Makazi hayo ni haramu chini ya sheria za kimataifa?

Jumuiya nyingi za kimataifa , Umoja wa kimataifa na mahakama ya haki kimataifa, zinasema kuwa makazi hayo yapo kinyume na sheria .

Wakisimamia makubaliano yalioafikiwa katika mkutano wa nne wa mwaka wa 1949 ambao unakataza utawala wowote kuhamisha watu kuwaweka katika eneo walilolipata baada ya vita.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Israel na Umoja wa mataifa wamekuwa wakipishana juu ya makazi ya wayahudi Yerusalemu

Hata hivyo Israel inasema kuwa makubaliano hayo ya Geneva hayawezi kutumika katika ukingo wa magharibi kwa sababu ya eneo hilo kiuhalisia halijachukuliwa .

Israel inasema kuwa ina haki kuwa nayo kutokana na matokeo waliyoyapata baada ya vita.Source link