Kevin de Bruyne amekuwa kiungo muhimu wa Manchester City msimu huu, akitengeza nafasi chungu nzima zaidi ya mchezaji mwengine yeyote mbali na kuongoza jedwali miongoni mwa wachezaji waliotoa pasi nyingi zilizosababisha magoli.

Ni ndoto ya mshambuliaji yeyote yule, kucheza mbele ya De Bruyne kutokana na pasi zake murua anazotoa. Anaweza kukupatia kile unachohitaji mbali na kwamba pia anaweza kufunga.

Goli lake dhidi ya Newcastle wiki iliopita lilikuwa bora zaidi – lakini sishangai anapofanya vitu kama hivyo ambazo ni ishara za mchezaji mzuri-anaweza kufanya kila mara.

Kevin de Bruyne ametengeneza nafasi 55 katika ligi ya Premia msimu huu.
De Bruyne ameandaa nafasi 37 kutoka maeneo mbali mbali ya uwanja mbali na kuandaa nafasi nyengine 18 kutoka kwa mikwaju ya adhabu, iki ni tatu zaidi ya mchezaji mwengine yeyote katika ligi ya Premia.

Sio lazima uwe bora ndio ufanye vizuri katika timu – kama alivyo kiungo wa kati wa Man United Scott Mc Tominay ambapo ameimarika na kuwa miongoni mwa viungo wa kati wazuri zaidi kuwahi kuichezea Man United.

Hawezi kufananishwa na wachezaji wengine katika kutengeneza nafasi za magoli lakini kwa sababu tofauti , atakuwa muhimu katika timu yake katika debi ya Jumamosi.

McTominay ndiye mtu anayetegemewa United

McTominay atakuwa mmojawapo wa majina ya kwanza katika kikosi cha United katika uwanja wa Etihad na mara nyengine alionyesha kwa nini siku ya Jumatano alishinda dhidi ya Tottenham.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uskochi alirudi baada ya mechi mbili za ligi ambapo alikuwa amejeruhiwa na kuleta nguvu nyingi katika safu ambayo ilikuwa hafifu.

Mkufunzi wa United alipongeza uongozi wake na uwezo wake na kusema ni mchezaji ambaye hawezi kuachwa nje baadaye na sasa naona kwa nini.

Scott McTominay na mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer
Baaada ya ushindi wa United dhidi ya Tottenham , Solskjaer alimzungumzia McTominayna kusema anataka kuwa mchezaji bora atakavyoweza. Huyu ndio mhezaji ninayemtaka katika klabu hii

McTominay amekuwa tegemeo kubwa sana kwake , katika eneo ambalo timu hiyo imekuwa hafifu na United itahitaji nidhamu na mipango katikati iwapo wanataka kuinyamazisha City.

City imekuwa na matatizo katika idara hiyo, huku Rodri akitumia muda mwingi kupata uzoefu katika jukumu lake la kuchukua nafasi ya Fernandinho kama kiungo wa kati.

Lakini Rodri alikuwa muhimu dhidi ya Burnley siku ya Jumanne usiku , hatua ambayo ni ishara nzuri kwa City kabla ya mechi ya wikendi.

Aliweza kuwazuia wachezaji wa timu hiyo mara kwa mara kila walipojaribu kupenya katika lango la City.

Walimuhitaji kwasasabu imekuwa rahisi kupita safu ya ulinzi katika mechi zilizopita.

Ni vyema kwa Guardiola ambaye anasema kwamba walishambuliwa mara mbili pekee na Newcastle siku ya Jumamosi lakini magoli yote yaliingia.

Mchezo wa City ulidhihirisha kitu .

Ilikuwa wiki njema kwa klabu zote mbili za Manchester na zote mbili zitaingia siku ya Jumamosi zikiwa na sababu za kuamini kwamba zitafanikiwa.

City walicheza kana kwamba wana sababu ya kudhihirisha dhidi ya Burnley siku ya Jumanne usiku na jinsi ‘walivyofurahia ilionyesha umuhimu wa mechi hiyo.

Kwa nini ushindi huo ulikuwa muhimu? , ukweli ni kwamba kila mtu anazungumzia kuhusu Liverpool na Leicester katika ushindani wa taji la ligi.

Ilifikia wakati ambapo klabu ya Guardiola ilikuwa imesahaulika katika kinyang’anyiro hicho na walikuwa nyuma na pointi 11.

Walikua hawajacheza vizuri katika kipindi cha wiki chache zilizopita na nikaona kwamba watakuwa na wakati mgumu wakicheza dhidi ya Burnley.

‘Ushindi wa Man United dhidi ya timu kubwa unawapatia matumaini’

Vilevile ushindi wa Jumatano dhidi ya Tottenham ulikuwa mkubwa kwa klabu kama United .

Kiwango cha mchezo wao kilikuwa kizuri na walionyesha mchezo mzuri kuanzia mwanzo.

Napenda jinsi walivyocheza dhidi ya Spurs kutoka mwanzo wa mchezo, na jinsi walivyopanda baada ya Tottenham kusawazisha na baadaye kuwazuia vizuri mwisho.

Hakuwakuweza kufanya vitu kama hivyo mara kwa mara katika majuma ya hivi karibuni. United wanaelekea katika uwanja wa Etihad wakitafuta kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya timu kubwa.

Mchezo wao mzuri dhidi ya timu bora za ligi ya Uingereza ni ishara tosha kwamba watafanikiwa.

‘City inaweza kutawala mchezo lakini United inaweza kutengeneza nafasi za magoli’

Kikosi cha Solskjaer bado hakijapoteza dhidi ya timu ambayo ilimaliza katika nafasi sita bora za ligi ya Uingereza na ni miongoni mwa timu mbili pekee ambazo zimefanikiwa kuilaza Leicester City 2019- 20.

Ushindi wao dhidi ya Spurs ndio uliodaiwa kuwa mzuri zaidi dhidi ya timu ambayo inafunzwa na mkufunzi wao wa zamani Jose Mourinho ambaye angewatia motisha wachezaji kwa mara ya kwanza akirudi katika uwanja wa Old Trafford tangu afutwe na Man United.

Ndio wanahitahi uzoefu kuthibitisha kwamba wanaweza kuzifunga timu ambazo hazina upinzani mkubwa.

Huku City ikitarajiwa kutawala mchezo siku ya Jumamosi , tisho la United katika uvamizi inamaanisha kwamba hawatajali.

United inapenda kucheza dhidi ya timu zinazpenda kuvamia na kushambulia lango lake kwa kuwa wana kasi ya kuwatia jeraha wanapovamia na nina hakika watapa nafasi Etihad.

Marcus Rashford alionyesha kiwango kizuri cha mchezo dhidi ya Spurs na alifanya kila kitu alichohitajika kufanya. Alionekana amenolewa na atajaribu kufunga magoli zaidi wikendi hii.

Zifahamu rekodi zao kabla ya mtanange wa leo.

Jumal ya michezo ya ligi waliyocheza ni 44 Man City wakishinda jumla yamichezo  15 nyumbani yaani wakishinda michezo  8 na ugenini yaani Old Trafford wakishinda michezo 7.

Kwa upande wa Man Utd wao wameshinda jumla ya michezo 21 ya ligi nyumbani wakishinda michezo 10 na ugenini wakishinda michezo 11, Je Leo mchezo ukipigwa Etihad nyumbani kwa Manchester City nani kuibuka mbabee?

By Ally Juma.Source link