Wasanii wawili kutoka Afrika, Rapper Burna Boy kutoka Nigeria na mchekeshaji Trevor Noah kutoka Afrika Kusini wametajwa kuwania tuzo za Grammy 2020 kwenye vipengele viwili tofauti tofauti.

Burna Boy na Trevor Noah

Rapper Burna Boy yeye ametajwa kwenye kipengele cha ‘Best World Music Album”  kupitia album yake ya African Giant.

Naye mchekeshaji, Trevor Noah yeye ametajwa kwenye kipengele cha ‘Best Comedy Album’ kupitia kazi yake ya ‘Son of Patricia’ .

Tuzo hizo kubwa kabisa duniani, zinatarajiwa kutolewa Januari 26, 2020 na host wa sherehe za ugawaji wa tuzo hizo atakuwa Alicia Keys.Source link