Michel PlatiniHaki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Michel Platini alikuwa mkuu wa Uefa kuanzia 2007mpaka alipopigw amarufuku mnamo 2015

Rais wa zamani wa Uefa Michel Platini anahojiwa na wachunguzi wa Ufaransa wa kupambana na ufisadi kuhusu kuipa Qatar fursa kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2022, shirika la habari Reuters linaripoti.

Waendesha mashtaka wanachunguza tuhuma za ufisadi na upokeaji hongo.

Platini, mwenye umri wa miaka 63, alikuwa kongozi wa shirikisho hilo la soka Ulaya mpaka alipopigwa marufuku mnamo 2015 kwa kukiuka maadili.

Mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa zamani wa Ufaransa na mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon d’Or daima amekana kufanya makosa yoyote.

Qatar iliishinda Marekani Australia, Korea kusini na Japan mnamo 2010 katika ombi la kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya kombe la dunia.

  • Fifa yabadili mpango wa Kombe la Dunia kuwa na timu 48
  • Kombe la Dunia 2022: Fifa imetakiwa kuifanyia uchunguzi wa ‘kipekee’ Qatar

Platini anahojiwa huko Nanterre, kitongoji kilichopo magharibi mwa mji mkuu Paris.

Maafisa wamekuwa wakichunguza tuhuma za ufisadi zinazohusiana na kombi la dunia 2018 na lijalo 2022 kwa miaka miwili iliyopita na inaarifiwa walimhoji aliyekuwa rais wa Fifa Sepp Blatter mnamo 2017.

Platini alipigwa marufuku kwa ‘malipo ya urongo’ ya £1.3m kutoka kwa rais aliyekuwepo wa Fifa Blatter, ambaye pia alipigw amarufuku kutoshirikia soka kwa kuhusika katika suala hilo.

Blatter pia amekana kufanya makosa yoyote.

Marufuku ya miaka minane ya mchezaji huyo wa zamani wa kiungo cha kati baadaye ilipunguzwa hadi miaka minne baada ya kukata rufaa na marufuku hiyo itamalizika Oktoba 2019.

Kikosi kilichowasilisha ombi la Qatar kinakabiliwa na tuhuma za rushwa, lakini kiliondoshewa mashtaka baada ya uchunguzi wa miaka miwili wa Fifa.Source link