Kile kilio cha muda mrefu kuhusu watu kulalamika akaunti zao kudukuliwa na kubadilisha majina na mwisho wa siku urudishaji wa akaunti hizo kuwa mgumu, Instagram imeamua kuleta msaada rahisi zaidi kwa yeyote yule atakuwa amedukuliwa akaunti yake.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa mtandao wa instagram akiuambia mtandao wa Motherboard, toleo hili la mtu kurejesha akaunti yake litafanyika ndani ya app ya instagram, mtumiaji ambae amedukuliwa atatakiwa kujaza email yake au namba ya simu na instagram itatuma tarakimu sita ambazo zitasaidia kurejesha akaunti yako, si hivyo tu, endapo mdukuzi atakuwa amedukua mpaka email yako na namba yako ya simu, instagram wanadai kuangalia kifaa cha meanzo ambacho ulitumia kutengeneza email yako.

Msemaji huyo alisema;-

“Tunajua kuwa kupoteza upatikanaji wa akaunti yako inaweza kuwa jambo lenye kutisha. Tuna hatua za kuacha akaunti 
pamoja na hatua za kuwasaidia watu kurejesha akaunti zao,” aliongeza “Lakini tuliposikia kutoka kwa jumuiya kwamba hatua hizi hazitoshi, na watu wanajitahidi kupata upatikanaji wa akaunti zao
“watu wanapatashida ya kufikia na kuzitumia akaunti zetu za Instagram.”

Toleo hili lipo kwenye majaribio kwa sasa ila linatajwa kutolewa katika kipindi hiki, hapo hutakuwa tena na hofu ya kutafuta wataalamu wa maswala ya kimitandao.

By Ally Juma.Source link