The little girlHaki miliki ya picha
Family handout

Image caption

Mtoto mchanga alikua bado hajapewa jina

Muuguzi wa dharura nchini Pakistan amekamatwa baada ya kudaiwa kumuiba mtoto mchanga ili ampelekee shangazi yake ambaye hakuwahi kuwa na mtoto.

Mtoto huyo mchanga wa kike aliibiwa muda mfupi tu baada ya kuzaliwa katika hospitali ya mji wa Balochistan, uliopo kusini- magharibi mwa nchi.

Lakini awali familia haikuwa unafahamu kuwa mtoto wao alitoweka kwasababu hakuna yeyote aliyemfichulia mama yake kuwa alikua amejifungua mapacha.

Ilijulikana kwa mara ya kwanza pale mama alipopata fahamu tena na kuuliza ni wapi aliko “msichana wake mwingine”, shemeji yake ameiambia BBC.

Abdul Hamid alikuwa amempeleka mama huyo mtarajiwa , Jamila Bibi, katika hospitali ya mji wa Loralai, yapata kilomita 60 (maili 37) kusini magharibi mwa kijiji chao, Jumatano, polisi wanasema.

Aliiambia polisi kuwa baada ya kujifungua, familia ya Jamila Bibi ilikabidhiwa mtoto mmoja na kuambiwa impeleke mgonjwa nyumbani kwasababu alikuwa na hali nzuri.

Unaweza pia kusoma:

Hata hivyo, Jamila Bibi aliendelea kuwa katika hali ya kutojitambua kwa siku kadhaa zilizofuata, na ni katika kipindi hicho ambapo mtoto aliyekwenda nae nyumbani alifariki.

Halafu – alipopata fahamu – mama huyo alifichua kile kilichoiacha familia vinywa wazi kwa mshangao.

“Ijumaa, wakati Bibi aliporejesha fahamu, aliuliza ni wapi alipo mtoto wake mwingine msichana. Tulishangaa.” Abdul Hamid aliiambia BBC.

Kukamatwa kwa mshukiwa

“Baada ya Abdul Hamid kuwasilisha malalamiko kwa polisi, tulimkamata mwanamke muuguzi wa dharura ambaye alikuwa zamu katika chumba cha uzazi usiku ule, na akatuongoza moja kwa moja kule alikokuwa mtoto mchanga,” Jahangir Shah, afisa katika kituo cha polisi cha Loralai alisema.

“Alikuwa amesaidiwa na manesi wengine wenzake wawili kumtorosha mtoto mchanga nje ya hospitali na kumpatia shangazi yake ambaye alikuwa ameolewa kwa miaka 17 lakini alikuwa bado hajapata mtoto. Muuguzi alituambia kuwa shangazi yake alikuwa ametaka sana kuasili mtoto mchanga.”

Polisi imewakamata wanawake wote wanne, huku familia ikiungana na mtoto wao mchanga, ambaye bado hajapewa jina.

Image caption

Wizi huo haukutarajiwa, wataalamu waliiambia BBC

Maafisa wanasema kuwa tukio hilo limetokana na ukosefu wa taratibu, kama vile kuweka majina kwenye mikono yaya watoto wachanga wanaozaliwa, na uzembe wa maafisa usalama katika milango ya kutoka kwneye hospitali hiyo.

Taktari bingwa wa uzazi wa wanawake katika hospitali ya Bolan Medical mjini Quetta, mji mkuu wa jimbo la Balochistan , aliiambia BBC kuwa tukio hilo halikutarajiwa , lakini ni sababu ya kuwa na hofia.

“Hakuna hospitali yoyote ya serikali katika jimbo yenye taratibu za usalama kama vile kuweka majina ya watoto wanaozaliwa au usajiri wao ambao unaweza kuthibitishwa wanapoondoka katika milango ya kutoka hospitalini ,” alisema, akiomba jina lake lisitajwe.Source link