Inakadiriwa kuwa kuna ombaomba 50,000 na zaidi ya makahaba 10,000 mjini Addis AbabaHaki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Inakadiriwa kuwa kuna ombaomba 50,000 na zaidi ya makahaba 10,000 mjini Addis Ababa

Maafisa katika mji mkuu wa Ethiopia Adis Ababa wanaandaa mkakati kupiga marufuku ukahaba na kuombaomba wa mitaani , ikiwa ni hatua ya hivi karibuni katika msururu wa hatua za kusafisha sura ya taifa , imesema ofisi ya meya wa mji huo.

Muswada unaoonyesha sheria za marufuku hizo bado unakamilishwa.

Hata hivyo afisa wa habari wa Meya wa Mji wa Adis Ababa Feven Teshome, ameliambia shirika la habari la AFP amesema marufuku hizo ni muhimu ili kupambana na “matatizo ya kijamii ” katika mji huo wenye zaidi ya watu milioni moja.

” Tunakadiria kuwa kuna ombaomba 50,000 na zaidi ya makahaba 10,000 mjini Addis Ababa. Muswada wa sheria unalenga kumaliza matatizo haya ya kijamii ambayo pia yanaleta picha mbaya kwa Ethiopia,” anasema Feven.

Kazi ya ukahaba kwa sasa si uhalifu nchini Ethiopia, na Feven anasema pendekezo la kuipiga marufuku mjini Addis Ababa itawahusu tu ombaomba wanaozurura mitaani.

Hii ikimaanisha kuwa haiwezi kutekelezwa katika sehemu kama vile baa , maineo ya kusinga, nyumba za malazi na maeneo mengine ambapo shughuli za ukahaba huwa ni nyingi.

Wafanyabiashara ya ukahaba na wateja wao kwa pamoja watakabiliwa na adhabu ambayo inaweza kuwa ni kulipa faini au kufungwa jela kwa muda fulani anasema Feven.

Image caption

Mhandisi Takele Uma, Naibu Meya wajiji la Addis Ababa

Marufuku pia itawahusu ombaomba wa mtaani na wanaowapatia pesa ombaomba.

Hata hivyo baadhi ya raia wa Ethiopia wamekuwa na hisia tofauti juu ya marufuku hii inayopangiwa makahaba na ombaomba jini Adis Ababa:

”Kusema kweli marufuku marufuku ingetolewa baada ya utafiti kufanyika, hakuna sheria inayozuwia ukahaba na ombaomba…hala fu jiji la Adis Ababa halikufanya matayarisho ya kukabiliana suala hili kabla hata ya kuandaa marufuku hii… kuna sababu nyingi zinazomfanya mwanamke awe kahaba hasa matatizo ya kiuchumi, hivyo mwanamke anapaswa kuwezeshwa ili asifanye biashara ya ukahaba” amesema wakili mjini Adis Ababa Seble Assefa,

  • Bugarama ”kitovu cha ukahaba” Rwanda
  • Wafungwa wataka kuongezwa mshahara Kenya

Mnamo Mei, maafisa wa Ethiopia walitangaza sheria kuhusu matangazo ya biashara ya pombe kote nchini ambapo walipiaga marufuku matangazo ya biashara ya pombe na sigara katika maeneo ya umma.

Sheria hiyo pia ilipiga marufukumauazo ya pombe kwa mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 21.

Image caption

Utawala wa mji wa Adis Ababa unasema makahaba na ombaomba hulipwa pesa nyingi jambo ambalo ni changamoto kwa mji kuwaondosha mitaani

Katika juhudi za kutekeleza masharti ya uvutaji wa sigara , katika miezi ya hivi karibuni vikosi vya usalama vilivamia vilabu vya pombe vya usiku ambavyo vilishukiwa kuuza shisha, au sigara za mvuke wa maji, sigara za kawaida , na kuwakamata kwa muda wateja na wahudumu.

Mwezi uliopita maafisa mjini Addis Ababa walizuwia usafiri wa pikipiki kwa lengo la kukabiliana na uhalifu.

Huku wakiandaa kuwasaka wafanyabiashara ya ukahaba na ombaomba wa mitaani , Feven anasema wanajaribu kutoa “fuhrsa ya kazi mbadala ” kwa watakaoathiriwa na marufuku.

  • ‘Sikutosheka kushiriki ngono mara 5 kwa siku’
  • Danguro ‘kubwa zaidi’ Asia lapata sura mpya
  • Papa Francis awataka makasisi Nigeria wamtii

Hata hivyo amebainisha wazi kuwa ukahaba na ombaomba ni kazi zenye malipo mazuri s , zinazowafanya zoezi la kuwaondosha mitaani kuwa gumu .

“Baadhi ya ombaomba hawa hupata hadi birr 7,000 (zaidi ya dola 200) na makahaba wanaweza kupata mapato ya juu zaidi kuliko mishahara ya kawaida ,” alisema Feven.

Mshahara wanaoupata kwa mwezi .

  • Ajikata kidole baada ya kukipigia kura chama asichokitaka

Maafisa wa jiji wanapanga kufanya mazungumzo zaidi juu ya sheria hiyo na viongozi wa kidini na kijamii kabla ya kuupigia kura muswadahuo wa sheria.

Suala la ukahaba limekuwa ni changamoto kwa miji mbalimbali barani Afrika, inayotaka iwe na sura ya maadili mema kwa wageni. Hata hivyo idadi ya makahaba imekuw aikiendelea kuongezeka, huku wengi wakidai wanaingia mitaani kufanya boiashara hiyo kutokana na hali mbali ya uchumi. Makahaba wengi wanaiona biashara hiyo kama njia ya kujiingizia pato linawasaidia kuendeleza maiasha yao na ya familia.Source link