Wengi miongoni mwa wakurugenzi wa makampuni waliofurushwa ni raia kutoka mataifa ya UlayaHaki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wengi miongoni mwa wakurugenzi wa makampuni waliofurushwa ni raia kutoka mataifa ya Ulaya

Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang’i ametia saini agizo la kuwarejesha makwao wakurugenzi 17 wa kigeni wa makampuni ya michezo ya kamari.

Agizo hilo limetekelezwa moja kwa moja, kwa mujibu wa ofisi ya rais.

Baadhi ya wakurugenzi hao walianza kuondoka jana kurejea makwao baada ya kushikiliwa kwa muda wa saa kadhaa kufuatia kusainiwa kwa agizo la Waziri wa mambo ya nje, yameripoti magazeti nchini humo.

Uamuzi wa kuwaondosha nchini ulifikiwa baada ya Kamati ya ushauri wa masula la kiusalama nchini Kenya (NSAC), ulioafikiwa na rais Uhuru Kenyatta, kuamua kuanzisha vita dhidi ya makampuni ya kamari.

Wengi miongoni mwa wakurugenzi wa makampuni waliofurushwa ni raia kutoka mataifa ya Ulaya mkiwemo Bulgaria, Italia, Urusi na Poland. Hata hivyo Wizara ya mambo ya ndani haijafichua majina ya wale waliofukuzwa nchini kwa madai ya kuhofia usalama.

Kabla ya kulazimishwa kuondoka nchini Kenya makampuni hayo yalikwenda mahakamani kupinga kuondolewa nchini kwa madai kuwa yalikuwa yametimiza masharti ya kuendesha biashara hiyo iliyoshamiri nchini Kenya. Hata serikali iliyashutumu makampuni hayo kwa kwa kukwepa kulipa ushuru mdogo, ikilinganishw ana mapato yake.

Image caption

Waziri wa mambo ya ndani wa kenya Dkt Fred Matiang’i

Kibali cha kuwarejesha katika nchi zao kilisema kuwa wamekuwa wakiishi Kenya kinyume cha sheria kwasababu vibali vya kuendesha kazi zao nchini Kenya vilikuwa vimefutwa.

Agizo hilo lilisema kuwa kazi zozote ambazo wanazifanya nchini Kenya ni kinyume na na vibali vyao vya kufanyia kazi.

Hatua hiyo ilikuja karibu zaidi ya mwezi mmoja baada ya kikosi cha maafisa kutoka mashirika mbali mbali kufanya uchunguzi wa leseni za makampuni yote ya michezo ya bahati nasibu nchini Kenya.

Iliripotiwa kuwa makampuni hayo ya bahati nasibu yalishindwa kuthibitisha kuwa yanalipa ushuru kulinga na maagizo ya Bodi ya Udhibiti na utoaji wa wa michezo ya bahari nasibu- Betting Control and Licensing Board (BCLB).

  • Makampuni ya kubeti matatani
  • SportPesa watoa udhamini kwa Serengeti Boys

Tarehe 11 Julai Serikali ya Kenya ilifuta vibali vya makampuni takriban 27 ya mchezo wa bahati nasibu hadi yatakapolipa ushuru. Miongoni mwa mambo yaliyobainiwa na Bodi wakati wa uchunguzi wake ni kwamba makampuni hayo yalipata faida ya shilingi bilioni 204 za Kenya mwaka jana, lakini yalilipa ushuru wa shilingi bilioni 4 pekee.

Jumanne asubuhi benki zilianza kufuja akaunti ambazo zinadhaniwa kuwa na mabilioni ya shilingi kufuatia agizo lililotolewa na benki kuu ya Kenya usiku wa Jumatatu.

Hatua ya kisheria

Image caption

Asilimia 76 ya vijana wa Kenya hushiriki michezo ya bahati nasibu pamoja na kamari

SportPesa, Betin na Betpawa zilikwenda mahakamani kutaka uamuzi uliotolewa awali na bodi ya udhibiti wa michezo ya kamari (BCLB) wa kuzuwia nambari za malipo ya wateja wao -paybill numbers na alama za siri.

Katika mashtaka yao, makampuni hayo yaliiomba mahakama ya juu kuwa biashara zao zimewekwa katika hatari ya kufungwa kwa kufanya kazi bila kibali nchini Kenya

Image caption

Kwa baadhi ya wachezaji, mchezo huo umegeuka kuwa uraibu

Pia walisema kuwa bodi ya BCLB ilifany amakosa kufunga nambari zao za malipo licha ya kwamba kesi ilikuwa bado inaendelea mahakamani.

  • JJe vijana Uganda wana uraibu wa mchezo wa kamari?

Hata hivyo hakimu alikataa maombi yao, ya kutaka maafisa wa BCLB waadhibiwe kwa kosa la kufuta vibali vyao vya kazi.

Makampuni yaliyofutiwa vibali vya kufanyanyia kazi nchini Kenya ni pamoja, SportPesa, Betin, Betway, Betpawa, PremierBet, Lucky2u, 1xBet, MozzartBet, Dafabet, World Sports Betting, Atari Gaming, Palms Bet na Betboss miongoni mwa makampuni mengine.Source link