Klabu ya Rangers International F.C maarufu kama Enugu Rangers inayoshiriki ligi kuu nchini Nigeria imejikuta ikiandika historia kwakuwa wa kwanza katika ramani ya soka kumtimuwa kazi kocha wao, Benedict Ugwu ilihali akiwa na timu uwanjani ikicheza.

Image result for Benedict Ugwu coach

Mara nyingi klabu huwamua kuachana na makocha mara baada ya mechi kumalizika ama inapokuwa katika maandalizi ya msimu, lakini hii ilikuwa ni tofauti na Enugu Rangers ambao wao hawakutaka hata kusubiri mchezo umalizike na badala yake wakamfungashia virago mwalimu wa timu hiyo hapo wakati kikosi chao kikiwa uwanjani kikitafuta pointi tatu muhimu mechi ya ligi kuu dhidi ya Akwa Starlet na kupelekea kupoteza kwa kipigo cha mabao 2 – 0.

Moses Praiz ambaye ni mtangazaji wa SuperSport alionekana kuguswa na tukio hilo na kusema kuwa hicho kilikuwa kitendo cha aibu ”Ni kitendo cha aibu, walipaswa wasubiri hadi mchezo umalizike ndipo wamwachishe kazi. Lakini sio kusimama ghafla na kumwambia umeachishwa kazi wakati ‘game’ ikiendelea,” amesema Moses

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Enugu Rangers ambayo kwa sasa ipo mkiani kwenye msimamo wa ligi kwakuwa nafasi ya 19 na pointi nne wakati anayeburuza akiwa na alama mbili peke nafasi ya 20, imempatia kazi mlindalango wa zamani wa Super Eagles goalkeeper Sylvanus Okpala kama kocha wao mpya.Source link