Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akizungumza wakati wa mkutano wa pande mbili na Rais wa Marekani Donald Trump huko Biarritz, kusini magharibi mwa Ufaransa Agosti 26, 2019Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Hatua iliyochukuliwa na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi imeongeza wasiwasi kwa walio wachache nchini humo hasa Waislam

Bunge la India limepitisha mswada wenye utata ambao utatoa msamaha kwa wahamiaji haramu kutoka nchi tatu jirani na India za Pakistan, Bangladesh na Afghanistan mradi tu wasiwe Waislamu.

Wanaharakati wanasema hii ni hatua ya hivi karibuni kuchukuliwa na mrengo wa Kulia wa chama tawala cha Bhartiya Janata Party kinachoongozwa na Narendra Modi miongoni mwa hatua zengine zilizochukuliwa.

Bwana Modi amekuwa madarakani tangu mwaka 2014 na kufanikiwa kuongeza idadi ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwaka huu.

Ingawa huenda Modi na chama chake wameendelea kupata umaarufu, baadhi ya sera zake zimekosolewa vikali kimataifa.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Narendra Modi ameendelea kupata umaarufu miongoni mwa raia wa India wanaoishi ughaibuni

Miongoni mwa yale ambayo amekuwa akikosolewa nayo ni pamoja na shutuma za kutenga walio wachache hasa Waislamu, ambao wanakadiriwa kuwa milioni 200 katika ya watu bilioni 1.3 wa India.

Haya ni baadhi ya maamuzi matatu ambayo yameendelea kuzua wasiwasi kwenye nchini hiyo ambayo idadi ya Waislamu ni ya pili kwa ukubwa duniani:

1. Mswada wa kufanyia marekebisho uraia

Mswada huo ulipitishwa na mabunge yote mawili nchini India ndani ya siku mbili na unalenga kutoa msamaha kwa wahamiaji haramu wasio waislamu kutoka kwa nchi tatu jirani Pakistan, Bangladesh na Afghanistan.

Wakati mswada huo sasa unasubiri Rais wa India kutia saini na kuwa sheria, chama tawala cha BJP kinasema kwamba kwanza kitafuatilia kwa haraka madai ya uraia kwa Wahindu, Wasikh, Wabuddhi, Wajaini, Waparsi, na Wakirsto waliotoroka mateso katika nchi jirani.

Sheria hiyo itapunguza miaka ya chini ya ukazi wa India inayomwezesha mtu kupata uraia kutoka miaka 11 hadi 6 lakini Waislamu wameondolewa katika kundi hili.

Hatua hiyo ambayo upinzani na wakosoaji wameichukulia kama inayopinga Waislamu, itakuwa mabadiliko ya kwanza ya uraia katika katiba ya India ambayo inakataza ubaguzi kwa misingi ya kidini.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mswada wa kurekebisha uraia umesababisha maandamano kote nchini India

Huku serikali ya Modi ikiwa imeapa kutobagua Waislamu na kusema kwamba wako salama nchini India, makundi ya Kiislamu na ya wanaharakati wa haki za binadamu yanasema hii ni hatua ya hivi karibuni inayotia wasiwasi Waislamu ambao idadi yao ni karibia milioni 200.

Sheria hiyo iliopendekezwa haiathiri raia waliopo India – Wahindu, Waislamu ama dini yoyote ile lakini itasaidia mamia na maelfu ya wahamiaji wa Kihindu walioingia India kutoka Bangladesh ambao bado hawajapata uraia.

Hii ndiyo sababu majimbo ya kaskazini mashariki mwa India yameshuhudua maandamano yanayopinga sheria hiyo mpya na kusema kwamba huenda idadi ya wahamiaji wasiowaislamu kutoka Bangladesh ikaongezeka na kuwazidi.

2. Ibara ya 370 ya Katiba ”Kashmir”

Jimbo la Himalayan huko Kashmir limekuwa chanzo cha mzozo kati ya India na Pakistan.

Kwa muda mrefu upande wa India umekuwa na wanamgambo na nchi hizo mbili zimeshuhudia mapigano mara kadhaa juu ya jimbo hilo la milimani.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Maandamano katika maeneo mengi yalishuhudiwa baada ya Ibara ya 370 ya katiba kufutwa, licha ya msako uliokuwa unafanywa na wanajeshi wa India

Wakati wa kugawanywa kwa India iliyokuwa inatawaliwa na Uingereza mwaka 1947, kulitokea vita kati ya India na Pakistan, na kuanzia hapo eneo la Kashmir likawa lenye kugawanya nchi hizo.

Lakini kulingana na katiba ya India ibara ya 370, inatoa uwezo wa kujitawala kwa jimbo la Kashmir lenye idadi kubwa ya Waislamu.

Mwaka 2019, chama tawala cha BJP kinachoongozwa na Modi, kiliamua kufuta ibara nzima ya 370 ya katiba na kusababisha hofu na maandamano.

Huku hadhi maalum ya kujitawala ya Kashmir ikiwa mjadala wa miaka mingi huko India, hakuna serikali hata moja zilizotangulia iliyowahi kubatilisha hadhi hiyo.

Lakini chama tawala cha BJP kiliondoa ibara hiyo ndani ya miezi kadhaa baada ya kuchaguliwa tena. Hatua hiyo ilifuatiwa na kufungwa kabisa kwa bonde la Kashmir shughuli iliyoongozwa na jeshi la India huku vyombo vya habari vikifungwa na mawasiliano yakakatizwa kwa miezi kadhaa.

Kwa raia wengi wa Kashmiri, Ibara ya 370 ya katiba ilikuwa ndiyo kithibitisho pekee cha eneo hilo kuwa chini ya India na kufuta ibara hiyo, chama cha BJP huenda kinajaribu kubadilisha idadi ya watu katika eneo hilo ambalo wengi wao ni Waislamu kwa kuwapa raia kutoka maeneo mengine ya nchi hiyo, haki ya kumiliki mali na kuwa na makazi ya kudumu katika eneo hilo.

Hatua hyo ilisababisha ghadhabu bungeni huku wataalam wa sheria wakiliita tukio hilo kama uvamizi wa katiba. Kesi ya kupinga hatua hiyo iliyochukuliwa na serikali ya Modi inasikilizwa katika Mahakama ya Juu Zaidi nchini humo.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Karibia watu milioni mbilib wa Assam wamevuliwa uraia

3. Sajili ya Raia

Sajili ya raia ni orodha ya wakaazi wote wa jimbo la Assam kaskazini mashariki mwa India ambao wanaweza kuthibitisha kwamba waliingia eneo hilo kabla ya Machi 24 1971, siku moja kabla nchi jirani ya Bangladesh kupata uhuru wake kutoka kwa Pakistan.

Sajili hiyo ilioundwa mwaka 1951 katika mchakato wa kubaini wahamiaji haramu ilipewa kipaumbele na serikali ya Modi.

Familia katika jimbo hilo wamehitajika kuthibitisha uzao wao na wale ambao hawawezi kuthibitisha wakichukuliwa kwama wahamiaji haramu.

Pia unaweza kusoma:Source link