Humphrey Polepole

Baada ya Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Mzee Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana kuandika waraka wakilalamika kudhalilishwa na Musiba, Hatimaye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole  amesema kuwa hajasikia wala kuona nakala ya waraka huo wa malalamiko.

Polepole akinukuliwa na gazeti la Mtanzania, amesema kuwa hajasikia wala kupata malalamiko hayo kwa kuwa kwa sasa yupo kwenye ziara vijijini.

Aidha, Polepole ameahidi kutoa msimamo wa Chama pindi tu atakapoupata waraka huo wa malalamiko ya udhalilishwaji ambao yeye amesema hajauona.

Waraka wa Mzee Yusuph na Kinana ulitolewa wiki iliyopita na wastaafu hao ukihoji kwanini, Mwanaharakati Musiba amekuwa akiwadhalilisha lakini Serikali haimchukulii hatua.

Image

Image

ImageSource link