Klabu ya Real Madrid wamefunga msimu wa 2018/19 kwa kukubali kipigo nyumbani cha goli 2-0 dhidi Real Betis na kuwafanya kumaliza na alama 68, Na kuweka rekodi kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 1995/96 ambapo walimal;iza La Liga kwa alama chache zaidi.

Bale na Zidane

Kufuatia kipigo hicho, Kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane amesema kuwa hatamtumia tena msimu ujao mshambuliaji wake, Gareth Bale .

Zidane amesema kuwa kwenye mchezo huu wa mwisho asingeli muingiza Bale, hata kama wachezaji wote wa sub wangeisha.

“Sitamjumuisha (Bale) kwenye kikosi changu cha msimu ujao, kuhusu mchezo huu kumuaga kwa heshima sikufikiria. Nadhani hata wachezaji wa ziada wangeisha nisingeweza kumuingiza uwanjani,” amesema Zidane.

Real Madrid wamemaliza msimu huu wakiwa nyuma ya alama 18 nyuma ya mabingwa wapya wa La Liga FC Barcelona.Source link