Baada ya kitendo cha kuwarushia fedha waandishi wa habari Jumatatu ya wiki hii, Hatimaye Muigizaji Irene Uwoya aitwa na kuhojiwa kwa kitendo hicho.

Irene Uwoya

Akithibitisha taarifa hizo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Camilius Wambura, amesema waliwaita wasanii wawili Irene na Steve Nyerere Juzi Jumatano Julai 17, 2019 na kuwahoji, kufuatia kitendo hicho.

Waliitwa kuja, walionekana kwenye clip moja, Yule Irene alionekana anatupa fedha, kwa wanahabrari, na alihojiwa na kudhaminiwa na uchunguzi mwingine unaendelea” amesema Kamanda Wambura.

Jumatatu ya wiki hii Julai 15, 2019. Irene Uwoya akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari aliwarushia hela waandishi wa habari, Jambo ambalo limetafsiriwa na watu wengi kama dharau ingawaje mwenyewe alikiri kosa hilo na kuelezea kuwa hakufanya kwa lengo baya, bali alitoa zawadi kwa waandishi.

 Source link