Rais aliyechaguliwa na wengi atahitaji washirika wengi bungeni kuhakikisha kwamba kuna upitishwaji wa haraka wa miswada mbali na kuidhinishwa maswala muhimu ya biashara za serikali iwapo mapendekezo ya BBI yatakubalika.

Kamati ya BBI inapendekeza kwamba rais atamchagua waziri mkuu, mawaziri na manaibu wao kutoka kwa wabunge waliochaguliwa kinyume na serikali ya sasa ilivyo ambapo mawaziri wanachaguliwa kutoka nje.

Fursa pia imetolewa kwa rais kuwachagua watu binafsi ambao sio wabunge lakini ambao watakauwa wabunge wa zamani, ikimaanisha kwamba wataruhusiwa bungeni lakini hawatakuwa na uwezo wa kupiga kura ili kuidhinisha miswada.Kulingana na ripoti hiyo waziri mkuu atachaguliwa miongoni mwa wabunge na lazima atoke kutoka chama chenye wanachama wengi katika bunge ama mtu aliye na ufuasi mkubwa iwapo kutakuwa na serikali ya muungano.

Rais atasalia kiongozi wa taifa na serikali mbali na kuwa kamanda mkuu wa jeshi. Yeye atakuwa kiunganisha cha umoja wa taifa.Rais atasimamia baraza la mawaziri , ambalo litakuwa na naibu wa rais , waziri mkuu na baraza la mawaziri.

Rais mwenye mamlaka atakuwa na uwezo wa kubaini sera za serikali kwa jumla huku mawaziri chini ya uongozi wa waziri mkuu watakuwa na jukumu la kuendesha biashara za serikali bungeni.

Rais ataongoza kwa awamu mbili kama ilivyo katika katiba. na naibu wa rais atakuwa mgombea mwenza wa rais . Naibu huyo wa rais atakuwa akimsaidia rais.

Jukumu la waziri mkuu:
Waziri mkuu atakuwa na jukumu la kuwasimamia mawaziri na kuhakikisha kuwa ajenda ya serikali inaeleweka ndani ya bunge na nje.

Kulingana na mapendekezo hayo mawaziri watakaokuwa na manaibu mawaziri pia watatarajiwa kutoka katika chama tawala ama muungano.Kiongozi huyo ataendelea kupokea mshahara wake kama mbunge na kwamba hakutakuwa nyongeza ya mshahara kwa jukumu lake jipya

Kufutwa kazi kwa waziri mkuu:
Waziri mkuu atafutwa kazi na rais ama kupitia kura isiokuwa na imani naye bungeni.

Mambo muhimu yaliyojitokeza katika Jopo hilo maarufuku kama ‘Handisheki’

  • Mpasuko mkubwa wa kisiasa umejitokeza nchini Kenya kuhusu maridhiano kati ya rais Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
  • Maridhiano hayo yameleta mgawanyiko ndani ya chama tawala cha Jubilee na muungnao wa upinzani unoongozwa na Raila Odinga wa NASA.
  • Naibu rais William Ruto anaongoza mrengo wa kisiasa ujulikanao kama Tangatanga” unaoonekana kupinga handisheki kati ya Uhuru na Raila.
  • Uhuru na Raila nao katika juhudi zao za kupigia debe maridiano yao ya kisiasa wana wafuasi wao wanaoegemea mrengo wa kisiasa wa Kieleweke.
  • Miongoni mwa vigogo wa muungano wa NASA wanaopinga handisheki ni Musalia Mudavaidi, ambaye ni kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC).

Hassan Joho: The problem lies between us. Say what you think is right. Diversity shall be our strength. Let us not shy away from saying the right thing. We should talk about building our nation #BBIReport

Posted by Citizen TV Kenya on Wednesday, 27 November 2019

By Ally Juma.

Source link