Nembo za bendera kwenye mavazi ya kijeshi

Image caption

Burundi na Rwanda zimekuwa zikishutumiana kuharibu hali ya usalama ya nchi zao

Shambulio lililotokea alfajiri ya siku ya Jumapili katika eneo la kijeshi la Burundi Kaskazini Magharibi, lilitokea siku nne baada ya shambulio la eneo la kijeshi nchini Rwanda karibia umbali wa kilometa 30 kuvuka mpaka wa Rwanda.

Mamlaka za nchi zote mbili awali zilishutumiana kwa kuingiza makundi ya wapiganaji kwa ajili ya kuvuruga amani.

Mkurugenzi wa habari wa Jeshi la Burundi Meja Emmanuel Gahongano amethibitisha kupitia Televisheni ya taifa kutokea kwa shambulio hilo bila kueleza zaidi, alisema ”washambualiaji walitoka na kurejea Rwanda”.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda ameiambia BBC kuwa ”si mara ya kwanza kunakuwa na shutuma hizi zisizo na msingi.

Hali hii imekuwa ikiendelea kwa miaka minne”.

Ni nini kilitokea kwenye shambulio hilo?

Eneo la jeshi la Burundi lilishambuliwa katika jimbo la Cibitoke eneo la ‘Twinyoni hill Mabayi’ lililo umbali ambao si chini ya kilomita 15 kutoka mpaka wa Rwanda karibu na msitu wa Kibira.

Chanzo kimoja katika jeshi la Burundi kimeiambia BBC idhaa ya maziwa makuu kuwa wanajeshi kadhaa waliuawa na kamanda kiongozi wa eneo hilo Meja Révérien Ngomirakiza, pia alipigwa risasi na kupoteza maisha.

  • Je Kagame na Nkurunziza watakutana DR Congo leo?

Huwezi kusikiliza tena

Rwanda,Uganda,Tanzania,Burundi na DRC kujadili jinsi ya kupambana na makundi ya waasi

Eneo lililoshambuliwa ni karibu umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la Jeshi la Rwanda karibu na msitu wa Nyungwe eneo la Bweyeye Kusini Magharibi mwa Rwanda eneo lililoshambuliwa na waasi usiku wa tarehe 8 mwezi Novemba.

Kundi la waasi wa Rwanda, FNL lilikiri kuhusika na shambulio hili, na kujigamba kuwa iliwauwa wanajeshi zaidi ya 20 wa Rwanda, msemaji wa Rwanda ameiambia BBC kuwa hakuwa tayari kuzungumzia hilo.

Mamlaka za Rwanda mwishoni mwa juma lililopita walitembelea eneo hilo na kusema kuwa washambuliaji hao wametoka nchini Burundi.

Mamlaka zimesema hivyo hivyo kuwa mwaka jana walishambulia Rwanda.

Hiki ni kisasi?

Msitu wa Nyungwe, ambao ni hifadhi ya taifa nchini Rwanda ina ulinzi mkali, sehemu ya msitu huu ambao unaelekea mpaka nchini Burundi katika eneo la Kibira pia linalindwa kuepuka waasi kupiga kambi na kuhatarisha hali ya usalama Burundi.

Kijiografia, makundi ya waasi wanaotoka DR Congo huvuka mpaka na kusafiri umbali wa kilometa 30 mashariki na kushambulia maeneo ya kijeshi bila kufukuzwa na vikosi vilivyo katika mpaka na DR Congo.

Inavyoonekana, majuma mawili yaliyopita makundi ya waasi wasingeweza kushambulia maeneo ya kijeshi ya Rwanda bila ya kupitia Burundi vile vile wasingeweza kufanikikiwa siku ya Jumapili kuikia maeneo ya Burundi bila kupitia Rwanda.

Nchi hizo mbili zimekuwa katika mgogoro tangu mwezi Aprili mwaka 2015 wakati serikali ya Burundi ilipoishutumu Rwanda kuunga mkono jaribio lililoshindwa dhidi ya Raisi Pierre Nkurunziza

Mahusiano yao hayajarejea kama kawaida tangu wakati huo, kuna hofu kuwa mvutano uliopo unaweza kuwa sababu ya mashambulizi ya hivi sasa kwa nchi zote mbili dhidi ya maeneo ya jeshi.Source link