ChanjoHaki miliki ya picha
GETTY IMAGES

Image caption

Mhudumu wa afya akitoa chanjo ya Ebola

Rwanda imezindua kampeni yake ya kwanza ya kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola. Zaidi ya watu elfu mbili na mia mbili wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika nchi jirani ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo tangu mwezi Agosti mwaka jana.

Waziri wa afya wa Rwanda, Diane Gashumba, alisema watu laki mbili wanatarajiwa kupata chanjo hiyo katika maeneo yanayopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kipaumbele kitapewa wafanyikazi wa afya, maafisa wa uhamiaji, polisi na wale wanaojihusisha na biashara ya mipakani.

Ni kwa nini Rwanda iliamua kutoa chanjo hiyo ilhali haijakabiliwa na ugonjwa wa Ebola?

Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola ilizinduliwa jana katika mji wa Rubavu kaskazini magharibi mwa Rwanda , mji unaopakana na mji wa Goma nchini DRC. kampeni hii itakuwa ikiendelea hata katika mji wa Rusizi kusini magharibi mwa Rwanda,mji unaopakana na mji wa Bukavu pia nchini Congo.

Rwanda haijakabiliwa na ugonjwa wa Ebola,lakini miji yake ya Rubavu na Rusizi inafanya biashara kubwa na nchi ya Congo,na ni miji yenye uingiliano mkubwa wa wananchi kutoka nchini mbili.

Jinsi chanjo zinavyookoa maisha yako

Je unaamini chanjo hufanya kazi?

Je kuna masharti yoyote ya watu kupewa chanjo hiyo?

Kulingana na wizara ya afya ya Rwanda ni watu 200,000 watakaopata chanjo hiyo,100,000 kutoka mji wa Rubavu na wengine 100,000 kutoka mji wa Rusizi.

Kipaumbele kitapewa wafanyakazi wa afya ,maafisa wa uhamiaji, polisi na raia hasa hasa wanaojihusisha na biashara ya mipakani,lakini pia wizara ya afya inasisitiza kwamba chanjo hutolewa kwa hiari ya kila mtu na mashrti yaliyopo ni kwamba chanjo inapewa mtu ambaye yuko tayari kupewa chanjo ya pili kwani ni sharti mtu apewe kinga mara mbili.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Dawa na bomba yenye sindano

Masharti mengine ni kwamba kwa wanawake wajawazito ni marufuku kupewa chanjo hiyo,na kwamba mwanamke atakayepewa chanjo ya kwanza atakuwa na uhakika kwamba hawezi kupata mimba katika kipindi cha kati ya chanjo ya kwanza na chanjo ya pili.

Kupata mimba ni mpaka kipindi cha mwisho wa chanjo zote mbili,ikikumbukwa kwamba chanjo ya pili hutolewa miezi miwili baada ya mtu kupata chanjo ya kwanza.Source link