An illustration of hands holding heartsHaki miliki ya picha
Getty Images

Ukarimu gani unaweza kuufanya? Je, ni sawa mtu kuonyesha hisia zao?

Inawezekana kuna ukweli , wanasayansi na wasomi katika kituo cha utafiti wanasema kuwa mtu anaweza kufanya mambo mengi zaidi ya ukarimu na kuongeza muda wa kuishi .

Wafanyakazi wa taasisi ya ukarimu ya Bedari iliyopo chuuo kikuu cha California, huko Los Angeles (UCLA) wako tayari kwa ajili ya utani.

“Tukiangalia upande wa kisayansi . Ni kama tuko kwenye mzunguko, hapa tunazungumzia upande wa kisaikolojia na kibaiolojia,” Daniel Fessler,mkurugenzi wa taasisi anaeleza.

  • Liberia yaongoza kwa Ukarimu kwa watu wasiowafahamu
  • Orodha ya nchi kwa ukarimu wa watu duniani

Suala la mtu kuwa mkarimu limeweza kuchukua vichwa vya habari hivi karibuni.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama anasema kuwa:

“Kuwa jasiri ni ukarimu. Hakuna ubaya kwa mtu kuwa dhaifu au kuwa na huruma,” alisema.

“Mtu kuwajali watu wengine si udhaifu. Ni jambo jema , tunapaswa kujali wengine kwa kuwa na uadilifu na kuwajali wengine kwa heshima.”

Ellen DeGeneres aliwahi kuzungumzia ukarimu wakati akizungumzia urafiki wake na George W Bush: “Ninaposema kuwa mkarimu, ‘Unapaswa kuwa mkarimu kwa wengine, simaanishi kama watu wanafikiria sawa na vile wanavyotenda. Ninachomaanisha ni kwamba uwe mkarimu kwa kila mtu bila kujali.'”

Leo ikiwa siku ya ukarimu duniani (Novemba 13) Tunaangazia ukarimu una maana gani – na kujiuliza kwa nini ni muhimu?

Hilo ndilo jambo ambalo wataalamu wanataka kufanyia utafiti.

Je wako makini , je ni suala ambalo linaingatia uhai na vifo vya watu.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Kazi ya bwana Fessler ilikuwa ni kuangalia namna ambavyo watu wanaweza kushawishika kufanya vitendo vya ukarimu, kwa kushuhudia fadhila na kueneza ukarimu.

“Nadhani ni sawa kusema kuwa tunaishi katika umri ambao sio rafiki,” alisema.

“Duniani kote , kile tunachokiona ni ongezeko la migogoro baina ya watu ambao wana maoni tofauti katika masuala ya kisiasa au tofauti za kiimani.”

Ukarimu, anasema kuwa ni “fikra, hisia na imani ambayo ina uhusiano na hatua ambazo zinaweza kuwanufaisha wengine, Kuwanufaifa wengine haimaanishi kuwa ndio mwisho.”

Na kutokuwa mkarimu kwa upande mwingine ni jambo ambalo lisilovumilika kutokana na watu kupunguza thamani kwa wengine.

Bwana Fessler anasema kuwa msongo wa mawazo ni miongoni mwa changamoto.

Kuishi na watu kwa wanakutendea vizuri ni bora, kuliko kuishi kwa hofu na mbaya zaidi kunafupisha maisha yako.

Kuishi na watu kwa ukarimu , na kuonyesha namna mtu anaweza kuwa mkarimu wa wengine kunasaidia mtu kupata tatizo la shinikizo la damu.

Kuna faida za kukabiliana na msongo wa mawazo na wasiwasi.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Ni rahisi kuwa mkarimu kwa wengine kuliko kwako mwenyewe

Mara nyingi huwa rahisi kuwa mkarimu kwa wengine kuliko kwako mwenyewe, anasema mtafiti .

“Kuna namna nyingi sana kuonyesha ukarimu kwetu binafsi na kwa watu wengine. Katika maeneo ya kazi , shuleni na nyumbani, ni maeneo ambayo mtu unaweza kuonyesha huruma na upendo kwa wengine”.

Katika sekta ya afya na teknolojia kuboresha lakini ukarimu hauwezi kuchukua mbadala wa namna ambavyo watu wanaweza kujali wengine.

Mahusiano kati ya afya ya akili na afya mwili ni mkubwa sana.”

Dondoo za kuwa mkarimu

  1. Anza kusikiliza wengine
  2. Jibu kwa upole na ukarimu
  3. Mjumuishe mtu ambaye anajitenga na wewe na kufanya vitu ambavyo vinaonyesha kuwa unawathamini na kuwapenda
  4. Chukua hatua na unapaswa kuelewa kuwa kuna watu ambao sio wakarimuSource link