Viongozi wa kijeshi nchini Sudani na muungano wa makundi ya upinzani wameunda rasmi baraza huru litakaloiongoza nchi hiyo kurudi kwenye utawala wa kiraia.

Protest leader Ahmed al-Rabie (2nd-R) alongside Lt-Gen Abdel Fattah Abdelrahman Burhan (C), head of Sudan's ruling Transitional Military Council during the signing ceremony in Khartoum on August 17, 2019, accompanied by General Hamdan Daglo "Hemeti" (2nd-L), TMC deputy chief and commander of the Rapid Support Forces paramilitaries, Ethiopian Prime Minister Abiy Ahmed (L), and Chadian President Idriss Deby (3rd-L)

Baraza hilo litaiongoza Sudani katika kipindi cha mpito cha miaka mitatu.

Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan ataliongoza baraza hilo kwa siku za awali. Wajumbe wa baraza ni raia sita na maafisa wa ngazi za juu watano wa jeshi.

Jenerali Burhan ndiye aliyechukua hatamu za uongozi baada ya jeshi kumng’oa Raisi Omar al-Bashir madarakani.

Baraza hilo linatarajiwa kuapishwa Jumatano (leo) asubuhi. Waziri Mkuu pia anatarajiwa kuapishwa hii leo pia. Hatua hiyo ilitangazwa na msemaji wa wa Baraza la Mpito la Kijeshi (TMC).

TMC ndiyo ilichukua mamlaka kutoka kwa Bashir mwezi April. Tokea hapo Sudan imeshuhudia maandamano ya kidemokrasia na pia mashambulizi makali ya waandamanaji kutoka kwa vyombo vya usalama.

Kwa nini hili linajiri?Hemeti

Baraza la utawala la jeshi nchini Sudani na muungano wa wapinzani walitiliana saini makubaliano ya kunda serikali mseto mwishoni mwa wiki.

Makubaliano hayo yalijumuisha uundwaji wa baraza huru, na kupokezana kijiti cha uongozi wa baraza baina ya jeshi na wapinzani.

Mwishoni mwa muda wa uongozi wao, baraza hilo linarajiwa kuandaa uchaguzi huru utakaorejesha utawala wa kiraia.

Jenerali Mohamed Hamdan “Hemeti” Dagolo, ambaye anatajwa kuwa ndiye mtu mwenye nguvu zaidi kwa sasa nchini Sudani ameahidi kuheshimu makubaliano hayo.

Mgogoro wa Sudani ulilipuka vipi?Sudanese President Omar al-Bashir addresses parliament in the capital Khartoum on 1 April 2019, in his first such speech after imposing a national state of emergency across on 22 February.Omar al-Bashir aling’olewa madarakani mwezi Aprili katika mapinduzi ya kijeshi

Hali ilianza kuwa tete mwezi Disemba 2018, pale ambapo serikali ya Bashir ilipotangaza hatua kali za kubana mkanda kiuchumi.

Makato kwenye bei ya mikate na bidhaa za mafuta yakazaa maandamano mashariki mwa nchi kupinga hali ngumu ya maisha, na hasira zikatapakaa mpaka mji mkuu wa Khartoum.

Maandamano hayo yakazaa matakwa ya raia kutaka utawala wa miaka 30 wa Bashir ukomeshwe.

Mwezi Aprili, Bashir akapinduliwa baada ya wiki kadhaa za waandamanaji kukita kambi nje ya makao makuu ya jeshi na wizara ya fedha.

Baraza la Majenerali chini ya Burhan likachukua hatamu, lakini limekuwa likabiliwa na changamoto kadhaa kuirudisha nchi katika hali ya kawaida.

Jeshi nchini Sudani lina matabaka; vikosi vya wanamgambo na makundi ya kiislamu wananguvu pia.

Wanamgambo wanaoongozwa na Hemeti (RSF) – ambao wametokana na kundi la Janjaweed ambalo linatuhumiwa kutekeleza mauaji katika jimbo la Darfur – wamekuwa wakilaumiwa kwa ghasia za hivi karibuni.

Ghasia hizo ni pamoja na mauaji ya Juni 3 ambapo watu 120 wanaripotiwa kuuawa, na wengi wao kutupwa kwenye mto Nile.

Hata hivyo viongozi wa RSF wamekanusha kupanga mauaji hayo, ambayo wanasema yalifanywa na askari waasi.Source link