Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ali Salehe Kiba alimaarufu Ali Kiba ameachia video ya wimbo mpya Mshumaa baada ya mashabiki wake kusubiria kwa muda mrefu.

Alikiba licha ya kuachia video ya wimbo huo pia alifanya listening party ya nyimbo kadhaa ambazo anatarajia kuziachia muda sio mrefu baada ya video ya mshumaa kufanya vizuri.

Katika mkutano na waandishi wa habari alikiba alimtambulisha msanii mpya wa l;ebo ya kings Music anayejulikana kwa jina la Tommy Flavour na kutangaza tamasha kubwa ambalo litaanza atakalolifanya kwa kuzunguka Tanzania nzima.

By Ally Juma.Source link