Everton wako tayari kuipa changamoto Arsenal kumuwania mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, ambaye anauzwa na klabu yake ya Crystal Palace kwa kitita cha pauni milioni 80. (Evening Standard)

Manchester United, Everton na Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Juventus kuhusu kumsajili Blaise Matuidi. (Le Parisien)

Manchester United wanaongeza jitihadi kumpata kiungo wa Lazio, mzaliwa wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic. (Mirror)

Inter Milan wanamtaka mchezaji wa Man United Lukaku.

Livepool inamtaka beki wa kushoto wa Augsburg Philipp Max, 25, (Sport)

Mchezaji wa Real Sociedad Diego LlorenteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa Real Sociedad Diego Llorente

Tottenham na West Ham wanamtolea macho Diego Llorente, 25 wa Real Sociedad. (El Mundo Deportivo)

Wolverhampton Wanderers wanataka kumsajili mshambuliaji wa Italia na AC Milan Patrick Cutrone mwenye thamani ya takriban pauni milioni 20. (Express & Star)

Tottenham imempa mkataba mpya wa mwaka mmoja mshambuliaji Fernando Llorente. (Mail)

Crystal Palace imetangaza dau la pauni la milioni 8 kumpata kiungo wa Everton James McCarthy. (Sky Sports)

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amemaliza matumaini ya Everton kwa kumsajili Kurt Zouma ambaye aliutumia msimu uliopita akiwa Goodison Park kwa mkopo. (Mirror)

Kocha wa Chelsea Frank Lampard
Image captionKocha wa Chelsea Frank Lampard

Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko, 33, huenda akaondoka Roma baada ya miaka mitatu, huku Inter Milan ikiwa na mpango wa kupata saini ya mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 15.(Sportitalia)

Mchezaji wa Chelsea, 18, Ethan Ampadu amefanya vipimo vya kiafya kabla ya kuhamia RB Leipzig ya Ujerumani. . (Sky Sports)

Klabu ya Brugge ya Ubelgiji ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Brighton na timu ya taifa ya Afrika Kusini Percy Tau, aliyecheza michuano ya kombe la mataifa Afrika. (Argus)

Derby County inataka kumsajili mlinda mlango wa Watford Daniel Bachmann, 25, kwa mkopo. (Derby Telegraph)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.Source link