TrumpHaki miliki ya picha
AFP

Image caption

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza na vikosi vyake Afghanistan

Rais wa Marekani Donald Trump amevitembelea vikosi vya Marekani nchini Afghanistan ikiwa ni ziara ya kushtukiza na kusema kuwa Marekani na Taliban wamekuwa katika mazungumzo.

”Taliban iko tayari kukubaliana,” Trump aliviambia vikosi katika kambi ya jeshi la angaa la Bagram, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini humo, ambapo pia alikutana na raisi wa nchi hiyo, Ashraf Ghani.

Ziara hiyo imekuja baada ya mpango wa kubadilishana mfungwa na mwanamgambo wa Taliban wakati wa kuanza kwa mazungumzo ya amani.

Bwana Trump amesema kuwa Marekani ilikuwa kwa kiasi kikubwa inapunguza idadi ya wanajeshi wake.

Wanajeshi 13,000 wa Marekani wanasalia nchini Afghanistan miaka 18 baada ya Marekani kuingilia kati kupambana na wanamgambo wa Taliban baada ya mashambulizi ya tarehe 11 mwezi Septemba mwaka 2001.

Ziara ya Trump inafanyika majuma kadhaa baada ya Taliban kuwaachia hutu wanazuoni wawili wa kutoka nchi za magharibi ambao walikuwa wakishikiliwa mateka tangu mwaka 2016, raia wa Marekani Kevin King na wa Australia Timothy Weeks wakibadilishwa na viongozi wa juu watatu wa wanamgambo hao.

”Tunakutana nao (Taliban) na tunasema lazima mapigano yakome na hawakutaka kukomesha mapigano na sasa wanataka kuweka silaha chini,” Trump alisema kwenye kambi hiyo iliyo karibu na mji mkuu, Kabul.” Ninaamini tutafanikiwa namna hiyo.”

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Trump akila chakula cha jioni na wanajeshi Marekani

Taliban ina mpango wa kufikia makubaliano?

Haijawa wazi ni kwa namna gani mazungumzo hayo yamekuwa na ukubwa kiasi gani.

Maafisa wa Afghanistan kwa muda mrefu wamekuwa wakitaka kumaliza mapigano lakini Taliban wanaodhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo tangu waondolewe mwaka 2001, wamekataa kufanya mazungumzo na serikali mpaka pale kutakapokuwa na makubaliano na Marekani.

Viongozi wa Taliban wamethibitisha kuwa mikutano na maafisa wa juu wa Marekani imekuwa ikifanyika mjini Doha tangu mwishoni mwa juma lililopita na kuwa mazungumzo rasmi bado hayajaanza, Shirika la habari la Reuters limeripoti.

  • Maisha ya Taliban ndani ya gereza kubwa Afghanistan
  • Mlipuko wa bomu wawaua watu 63 harusini

Trump amerejea kueleza mpango wa kupunguza idadi ya wanajeshi kufikia 8,600 lakini hakueleza ni wanajeshi wangapi watasalia huko au wataondoka lini. ” Tutaendelea kuwepo mpaka tutakapokubaliana, wana shauku kubwa ya kufikia makubaliano.”

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Trump akiwahudumia chakula wanajeshi wake

Raisi Ghani amevishukuru vikosi vya Marekani ”vilivyojitoa kwa kiasi kikubwa” nchini Afghanistan, akisema: ”Vikosi vya Afghanistan kwa sasa vinashika usukani.”

Akizungumzia mkutano huo kwenye ukurasa wa Twitter, Bwana Ghani hakugusia kauli ya Trump kuhusu mazungumzo yake na Taliban na kusema: ”Pande zote mbili zimesisitiza kuwa ikiwa Taliban kweli zinahitaji kufikia makubaliano ya amani lazima wakubali kuweka silaha chini.”

Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Taliban, na wengi awali walikuwa na maswali kuhusu utayari wa kundi hilo kujihusisha na mazungumzo hayo au kama wanaweza kuaminiwa.

Kilichotokea kwenye mazungumzo ya amani

Mazungumzo na Taliban yalivunjika mwezi Septemba muda mfupi baada ya Trump kuwaalika viongozi wa juu wa Taliban na rais Ghani nchini Marekani.

Lakini mashambulizi ya Taliban mjini Kabul siku mbili kabla, ambalo liligharimu maisha ya mwanajeshi mmoja wa Marekani na wengine 11, lilimfanya Trump kutoka kwenye mazungumzo hayo akisema Taliban ”Pengine hawana nguvu za kuzungumza” kama hawakuwa tayari kukubali kusitisha mapambano wakati wa mazungumzo.

Bwana Ghani amesema kubadilishana kwa wafungwa kulikofanyika mwezi huu kuna lengo la ”kufungua milango ya mazungumzo ya moja kwa moja ya amani.” Hata hivyo, Taliban kwa muda mrefu wamekataa kukubaliana na utawala wa Ghani, wakimuita kibaraka wa Marekani.Source link