Rais wa Marekani Donald Trump amesaini muswada wa kuunga mkono vuguvugu la maandamano ya kudai demokrasia mjini Hong Kong na kuwa sheria licha ya pingamizi kutoka kwa serikali ya China.

Image result for trump vs china president

Sheria hiyo ambayo iliungwa mkono kwa sauti moja bungeni, inahitaji Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuthibitisha angalau kila mwaka kwamba uhuru wa Hong Kong haukutatizwa.

Kwa mujibu wa Deutsche Welle, Bunge la Marekani pia limepitisha muswada wa pili – ambao Rais Trump pia ameusaini – unaopiga marufuku usafirishaji na uuzaji wa silaha za kudhibiti maandamano ya umma kwa vikosi vya usalama vya Hong Kong kama vile, mabomu ya kutoa machozi, dawa ya pilipili, risasi za mpira pamoja na bunduki za kutoa mshtuko wa umeme.

China ilimuonya Trump wiki iliyopita kuwa itachukua hatua za kulipiza kisasi iwapo atasaini miswada hiyo na kuwa sheria, lakini hilo imeonekana kutupiliwa mbali na rais huyo wa Marekani na kuamua kusaini muswada huo.Source link