Andy Ruiz amrushia busu mwanawe . Amekuwa bingwa wa dunia na kutupilia mbali hali mbaya ya maisha waliokuwa wakipitia. Mkufunzi wa Ruiz Manny Robbles anaonekana akibubujikwa na machozi, akielekeza vidole vyake mbinguni na kupongeza uongozi wa babake aliyempoteza miaka 12 iliopita.

Hii ndio ndoto yetu

Umbali kidogo wa kutembea ni chumba cha maandalizi cha ukumbi wa Madison Sqaure Garden , Anthony Joshua anaambiwa na baba yake kwamba ni sharti arudi nyuma na kuangazia ni wapi alipokosea.

Rafiki wa karibu wa Joshua david Ghansa anaonekana akijivuta machozi.

Hii ilikuwa ndoto mbaya

Wiki ya kwanza ya pigano kati ya Joshua dhidi ya Ruiz ilianza huku raia huyo wa Mexico akionekana akitema mate juu ya dari ya jumba moja refu mjini Manhattan huku akisubiri mahojiano.

Tabia hiyo yake ya kutojali ndio kitu alichotumia katika siku zilizofuata huku idadi kubwa ya mashabiki wakimdharau.

Wiki mbili baadaye anaonekana ameketi kando ya rais wa Mexico akipongezwa kwa kuwa shujaa wa taifa.

Usiku huo ulimpatia hadhi hiyo – alipomshinda bingwa wa ndondi wa uzani mzito duniani Anthony Joshua ambaye alikuwa hajawahi kushindwa maisha yake yote – kitendo kilichowashangaza wengi na kuwatia wengine hofu.

 

Wiki moja kabla wawili hao kukutana tena katika pigano la marudiano , BBC Sport inakuangazia yale yaliokuwa yakiendelea nyuma ya pazia mnamo tarehe mosi mwezi Juni kupitia usaidizi wa wale waliohusika.

Short presentational grey line

Ni mwendo wa saa kumi na mbili jioni mjini New York . Klabu ya Liverpool imetoka kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya katika fainali ilioshirikisha timu mbili za England.

Lakini ushindi wao ukaondolewa katika tovuti kubwa duniani kutokana na kile ambacho wengi hawakutarajia kitafanyika.

Mbali na kwamba Jina la Ruiz halikuorodheshwa katika baadhi ya tiketi za mashabiki waliopiga foleni kuingia katika ukumbi wa Madison Square Garden kwa kuwa aliorodheshwa katika dakika za mwisho kuchukua mahala pake Jarell Miller.

Picha ya maumbile ya Joshua yenye misuli mingi imewekwa katika mabango huku raia huyo wa Uingereza akiwa amevaa tishati ya mitindo.

Saa 24 awali , baadhi ya watu matajiri walidhani kwamba Ruiz mwenye maumbile ya mtu aliyenona hatovua tisheti yake .

Hili ni pigano la kulipwa na mafuta ya ziada hayamfanyi mtazamaji kuona kwamba kutakuwa na pigano lenye ushindani wa hali ya juu.

Huku pigano hilo likikaribia , Ruiz anaonekana akifanya mambo katika chumba chake cha maandalizi halafu anaingia ulingoni na kusubiri

Baadaye Joshua anaingia ulingoni , kabla ya mashabiki waliojaa katika ukumbi huo hawajamuona anaonekana akijikumbusha kuhusu maelezo muhimu akisema:, kujilinda na kurusha ngumi kwa utulivu.

Ukumbiwa ndoni wa Madison Square GardenJoshua, mwenye umri wa miaka 30 alikuwa akipigana kwa mara ya kwanza katika ukumbi uanojulikana kama mecca ya ndondi.

Nyuma ya ukumbi huo Callum Smith anaonekana akifanyiwa vipimo vya dawa za kulevya baada ya kutetea taji lake .

Waliokuwa wakimpima walikuwa wakitizama pigano hilo la Joshua katika runinga na kutoa mzaha , wakisema: Nadhani pigano hili litakamilika kwa haraka zaidi ya pigano lako, anaambia BBC.

Wapimaji hao wameona kwamba Ruiz ameangushwa , kabla ya kusimama na kumuangusha Joshua mara mbili kufikia mwisho wa raundi ya tatu.

Utakapompiga utapunguza makali yake , Joshua anaambiwa na mkufunzi wake Rob McCracken. Upande mwengine , sekunde chache kabla ya raundi ya saba Robles anasikika akimwambia Ruiz:

”Je wajua ulimuumiza , hivyobasi endelea kupiga kichwa chake. Mburudishaji wa Uingereza James Corden anasikika kando ya ulingo akisema Joshua piga huyo, lakini katika kipindi kirefu pia yeye ameduwaa kama wengine waliokuwa naye. David Haye hawezi kuketi chini, kutokana na hasira za ripota aliyekaa nyuma yake.

Huku pigano hilo likiendelea, bingwa huyo wa zamani wa uzani mzito duniani ndiye mtu wa pekee anayesimama na kuanguka zaidi ya mtu anayemshabikia katika ulingo wa ndondi.

Mara Joshua akaangushwa mara ya tatu na nne mfululizo katika raundi ya saba, huku watu mamilioni wakitazama kwa mshangao yaliokuwa yakiendelea.

”Nilihisi nimekufa ganzi kwa kweli”,alisema Promota Eddie Hearn.

Nimeona mengi katika ndondi – majeraha, majanga, panda shuka . Unaweza kufa ganzi lakini kulikuwa na kitu kisichoweza kuaminika .Joshua amepigwa, amepiga goti moja katika kona yake . Ana taulo imewekwa juu ya kichwa chake. Meneja wake wa muda mrefu Freddie Cunningham amesimama mbele yake akiwa na wasiwasi katika uso wake.

Sahau kuhusu michezo, kuona mtu unayemjua akiwa asilimia 100 kuna wasiwasi mkubwa. Kulingana na maneno ya Cunningham , mambo huonekana kufanyika kwa kasi ndani ya ukumbi zaidi ya ndani ya uwanja – na pigano hilo lilifanyika kwa kasi kubwa.

Uvumi baadaye ulizunguka kwamba Joshua alikuwa mgonjwa na kwamba alikuwa amezirai kabla ya pigano hilo, lakini kundi la washirika wake walikana madai hayo .

Babake alikuwa ndani ya ulingo akimkosoa Eddie Hearn.

Ruiz anatoka katika ulingo wa ndondi akiwa amebeba mataji yote yaliokuwa na Joshua huku akipongezwa .

Umeushangaza ulimwengu. Ulimwengu wote unakupenda. Bondia huyo mwenye uzani wa kupitia kiasi ambaye hakuwa na matumaini kwa jina la utani ‘Destroyer’ kwa sababu ya kuvunja vitu utotoni mwake alikuwa chuma cha kuotea mbali.

Andy Ruiz Jr na mikanda yake aliyoshindaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRuiz, ambaye atakuwa na umri wa miaka 30 mwezi Septemba alizaliwa katika eneo la Imperial, California

Bondia wa Uingereza Smith anaandaa mkutano wake na vyombo vya habari, huku waandishi wakijazana katika chumba chake, baada ya pigano hilo la Joshua mita chache kutoka hapo.

Kamera zinawekwa , watu wanazungumza katika simu zao wengine wanauliza kule aliko Joshua na kuna habari kwamba anafanyiwa vipimo vya mshutuko.

Nilihisia vibaya. nakumbuka nikifikiria kwamba hakuna mtu anayejali kile ambacho ninakaribia kusema , anakumbuka Smith.

Nilihisi kana kwamba kuna mtu amefariki wakati mwengine. Ruiz anaingia akipongezwa. Mtu mmoja anasikika akipiga kelele Bingwa yuko hapa.

Hearn anasikika akizungumza katika ukumbi huo huku akionekana kana kwamba ameshtushwa na matokeo hayo. Rafikize kutoka Uingereza wanamtumia ujumbe wakimuuliza iwapo yuko sawa.

Lazima uzingatie , nina kazi ya kufanya, anakumbuka. Ruiz anamwambia mamake kwamba anampenda, na mamake anarejesha maneneo hayo matamu kwa kumrushia busu la upendo.

Mkufunzi wake ambaye ni mtu anayesema kwamba aliwasili nchini Marekani kama mkimbizi akiwa mtoto, anaonekana akibubujikwa na machozi.

Alimpoteza babake , kazi na nyumba 2007. Maswali kuhusu babake ambaye alipenda ndondi sana yalimfanya abubujikwe na machozi.

Anthony Joshua

Kulikuwa na kimya kirefu , Na wakati mmoja lifti iliwasili , milango ikafunguka kabla ya Ruiz na watu wake kutokea , wakicheka na kutabasamu.

Kulikuwa na kimya chengine kirefu ,Anthony Joshua alikuwa wa kwanza kutoka kupitia mlango wa nyuma wa chumba cha maandalizi, alitulia kwa muda na baadaye akatabasamu aliponiona.

Nilimuuliza swali la kwanza huku tukijaza lifti hiyo. Tukisalia katika mkutano na wanahabari , Ruiz anaondoka na vyombo vya habari vinaambiwa kwamba Joshua hatohudhuria mkutano huo na waandishi wanasubiri na wanaambiwa tena na tena.

Muda mchache wanaanza kuondoka. Joshua alipata mshtuko na daktari akamwambia asifanye mkutano na vyombo vya habari , alisema Hearn.

Alipooga na kuniona alisema kwamba atazungumza na vyombo vya habari , Nilikuwa namwambia asizungumze na wanahabari kupitia ujumbe na mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wanahabari wanasikia kwamba Joshua atakuwepo katika mkutano na vyombo vya habari , wanakimbia wakirudi lakini walinda usalama wanasema kwamba hakuna anayeruhusiwa kuingia katika ukumbi huo maarufu.

Lakini baada ya maelezxo marefu wanangia na kumpata bingwa wa zamani ambaye amekataa kushindwa. Joshua anauelezea usiku huo kama usiku mfupi sana huku baadhi ya washirika wake wakiwa wameketi kando yake wakiweka vichwa katika mikono yao .

Ruiz asherehekea baada ya ushindi dhidi ya JoshuaRuiz alichaguliwa katika dakika za mwisho kuchukua mahala pake Jarell MIller ambaye alipatikana na dawa za kusisimua misuli

Wengine wakiwa wametegemea migongo yao na kutazama juu.

Ulikuwa usiku mgumu, alisema mkufunzi wake Robert McCracken. Ilimchukua Joshua kipindi kirefu kabla ya kurudia hali yake lakini tulifanya uamuzi wa pigano la marudio haraka.

Ruiz kama alivyofanya wakati wa pigano kubwa zaidi katika maisha yake alikuwa akitabasamu huku akisimama nyuma ya gari lake aina ya Rolls Royce katika mji wa California.

Wiki moja kabla alikuwa amesimama juu ya jumba refu la New York akiwa amevalia suruali ndefu aina ya Jeans akiwa ameingiza mikono yake ndani ya suruali hiyo.

Hakuonekana kwamba atakuja kuwa bingwa lakini baada yake siku sita alikuwa bingwa. Alikuwa na usiku wa maisha yake . Ni usiku ambayo ulimwengu wa michezo hautausahau kwa haraka.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.Source link