Atheris Viper (Bush Viper)

Kukiwa na misitu mingi, makazi ya viumbe aina ya nyoka wengi wenye sumu, DRC ni eneo ambalo misitu yake imekuwa ikigharimu watu kwa majeraha na vifo kutokana na kuumwa na nyoka wenye sumu, suala ambalo limeelezwa na Shirika la afya duniani, WHO na Shirika la madaktari wasio na mipaka, Médecins Sans Frontières wakisema kuwa hatari hii imekuwa ikipuuzwa Afrika.

Mpiga picha Hugh Kinsella Cunningham amekuwa akiweka rekodi na kupiga picha za karibu za baadhi ya nyoka hatari zaidi duniani.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Mvuvi Patrick Atelo anamuonyesha aina ya nyoka aliye hai, aitwaye Mamba kwenye mto Ruki.Nyoka alipatikana karibu na kijiji na, kwa sababu ya vifo vitokanavyo na kuumwa na nyoka, viumbe hao huwapa hofu na mara nyingi huuawa mara tu wanapoonekana.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Watu milioni 2.7 huumwa na nyoka wenye sumu kila mwaka, hali inayosababisha vifo vya watu kati ya 81,000 na 137,000, huku wengine wengi wakiishia kukatwa viungo na kuwa na ulemavu wa kudumu, kwa mujibu wa Ripoti ya WHO.

Nyoka mwenye macho matatu agunduliwa

Hakuna anayethubutu kumchezea Kasuku huyu

Miaka ya mizozo na rushwa zimedhoofisha miundo mbinu na hii ina maana kuwa dawa za kupambana na sumu zimeadimika au ni vigumu kuzisambaza.Kutokana na muingiliano kati ya maeneo yenye nyoka wenye sumu na watu waishio maeneo ya kijijini, imekua vigumu kufikia huduma za kiafya kwa urahisi hali ambayo imekua ikihatarisha maisha yao.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Nyoka hunaswa kwenye nyavu za wavuvi kwenye mto Congo, hivyo kunakuwa na uangalifu mkubwa wakati wakutazama kama wamenaswa.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Cunnigham pia alimpiga picha nyoka aina ya Cobra, kama huyo hapo juu.

”Kwa kuhakikisha kunakua na mazingira tulivu,niliweza kupata picha ya nyoka nikiwa umbali wa futi kadhaa na mahali walipo nyoka,” alisema.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

”Picha nyingine zilipatikana wakati nyoka walipokuwa wakichunguza lenzi ya kamera.Na nikahisi kuwa ilikua muhimu kuwapiga picha si wakiwa kwenye vizimba au ndani ya kioo bali wakiwa wanatembea huru, kama wanavyokuwa kwenye mazingira yao ya asili”.Cunningham anaeleza.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Joel Botsuna, ni afisa kutoka taasisi ya uhifadhi mazingira katika eneo la Ikweta amembeba nyoka aina ya mamba.Nyoka aliuawa na wakulima majira ya usiku.

Mamba ni nyoka aliye na sumu kali sana-sumu yake husababisha kifo ndani ya muda mfupi wa saa mbili baada ya kung’atwa.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Cobra ambaye ameingia kwenye mtego wa samaki unaomilikiwa na Shadrack Ifomi.Amekua akivua samaki maisha yake yote na amekua aking’atwa na Nyoka mara nyingi lakini bahati nzuri na nyoka wasio na madhara

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Mmiliki wa kiwanja aliumwa na nyoka alipokuwa akitembea kwenda kukagua mali zake.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Tabibu wa kienyeji katika mji wa Magharibi wa Mbandaka anaonyesha dawa za kutibu jeraha la kuumwa na nyoka.Mitishamba na kichwa cha nyoka hupondwa mpaka kutoa poda kisha huchomwa moto kabla ya kupakwa kwenye jeraha palipochanjwa na wembe kwa aliyeumwa na nyoka.

Dawa hizi zinaweza kusababisha athari.Kwa mfano kuchanja kwa kutumia wembe na kupaka vitu kwenye jeraha kunaweza kusababisa maambukizo

Mitishamba hukusanywa na matabibu kama Bienvenue Efete kwenye picha ifuatayo.

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella Cunningham

Dokta Anaurite Nyaboleka, anafanya kazi katika kituo cha afya cha Mbandaka.Yeye hawezi kupata dawa za kupambana na sumu, hivyo amebaki na uwezo wa kutibu dalili za maradhi yanayotokana na kuumwa na nyoka.

Nyama ya nyoka pia huliwa kama inavyoonekana kwenye soko la Makila, mjini Mbandaka.Nyama ya Nyoka huuzwa kwa pauni 2.40

Haki miliki ya picha
Hugh Kinsella CunninghamSource link