Picha hii inaonyesha mkono mmoja ukiushika mkono mwengine

Utafiti uliofanywa na BBC katika ulimwengu wa Waarabu ulitoa matokeo ambayo hayakutarajiwa nchini Iraq- ambapo wanaume zidi ya wanawake wamenyanyaswa kingono .

Je huu ni ukweli?

Sami ana umri wa miaka 13.

Yuko chooni shuleni ambapo wavulana watatu wakubwa zaidi yake walio kati ya umri wa miaka 15 na 17 wanamzuia kwenye ukuta .

Wanaanza kumtomasa baadhi ya maeneo ya mwili wake. Sami anashangaa na baadaye anapiga kelele.

”Nilianza kupiga kelele”. Mvutano huo uliwavutia watoto wengine ambao walimuita mwalimu mkuu. Vijana hao walifukuzwa shuleni: Lakini wazazi wao hawakuelezewa kiini cha kumshambulia kijana huyo.

Sami (sio jina lake ) baadaye aliitwa katika afisi ya mwalimu mkuu.

Kilichotokea baadaye pia kilimuathiri-kama shambulio la pili.

Aliambiwa kwamba shule hiyo itakichukulia kitendo hicho kama kisa cha kujamiana na kwamba alikuwa na bahati hakufukuzwa shule pamoja na waliomshambulia.

Sami alipewa fursa nyengine ya kuendelea na masomo.

”Kila mtu alidhani kwamba nilikuwa nikishirikiana na washambuliaji hao” , anasema.

Huku akiwa anatetemeka asijue cha kufanya kufuatia shambulio hilo, Sami aliamua kutowaambia wazazi wake na kusitisha mawasiliano na kila mtu kwa miezi kadhaa.

Hii ndio mara ya kwanza Sami alinyanyaswa kingono.

Sami ana umri wa miaka 15.

Mwaka 2007 babake alikuwa amefariki yapata mwaka mmoja uliopita. Kufariki kwa baba yake ambaye ndiye aliyekuwa akiwasimamia lilikuwa pigo kwa familia.

Alikulia katika mji ulioko katika mkoa wa Babylon nchini Iraq yapata kilomita 100 kutoka kusini mwa Baghdad.

Sami alikuwa na utoto uliojawa na furaha. Alikuwa akiamka saa moja afajiri akielekea shule na kurudi saa nane.

Sam alikuwa akisoma kwa muda mrefu na baadaye kutumia muda uliosalia na nduguye na dadake.

Jioni familia yake ilikuwa ikimtembelea babu yao kwa chakula cha jioni. Mara nyngine alikuwa akitoa usaidizi katika duka ambalo babake alikuwa akifanya kazi. l

Lakini kifo cha babake kilimaanisha kwamba Sami alihitaji kwenda kutafuta kazi.

Alipata kazi ya kuuza duka katika soko lililopo anakoishi. Na hapo ndipo alikumbwa na kisa kingine.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Sami alihisi hana raha kutokana na vile alivyokuwa akitazamwa sana na mmiliki wa duka hilo.

”Alinitunza sana”. anasema. Na siku moja walipokuwa peke yao , mmiliki wa duka hilo alimshika kwa nguvu na kujaribu kumpiga busu na kumkumbatia.

Sami alikataa na kushika bilauri ya kupanda maua iliokuwa karibu yake . Alimpiga nayo katika kichwa na kutoroka.

Sami hana uhakika ni nini mmiliki huyo wa duka aliiambia jamii lakini ilimchukua takriban mwaka mmoja kabla ya yeye kupata kazi nyengine.

Sami akiwana umri wa miaka 16.

Mamake na nduguze hawapo nyumbani na binamu yake amemtembelea. Akiwa ameketi karibu na Sami binamu yake anachukua simu yake na kuanza kutazama picha za ngono mbele yake.

Na mara moja anamshika kwa nguvu anamshinda nguvu na kumbaka. shambulio hilo la utumiaji wa nguvu lilikuwa la uchungu mwingi kwa Sami kulizungumzia.

Anapolifikiria sana linamuathiri na kumsababishia njozi mbaya.

Sami hakuweza kusalia katika makaazi yao. ”Nilifanikiwa kuwaraia wazazi wangu kuhamia kwengine. Tulivunja uhusiano na jamaa pamoja na rafiki zetu”, anasema.

Familia hiyo ilielekea Baghdad ambapo wote walipata kazi. Akiwa mjini humo alijenga urafiki na vijana majirani .

Alichogundua ni kwamba hakuwa pekee katika kile alichofanyiwa. Vijana wengine walimwambii kwamba hata wao walinyanyaswa kingono.

Utafiti uliofanywa na idhaa ya BBC Arabic katika mataifa 10 pamoja na maeneo ya Palestina ulibaini kwamba kati ya mataifa mawili Tunisia na Iraq wanaume walikabiliwa sana na unyanyasaji wa kingono zaidi ya wanawake.

Nchini Tunisia idadi hiyo hatahivyo ilikuwa ndogo kwa asilimia moja huku Iraq ikiwa kubwa. Hapa asilimia 39 ya wanaume walisema kuwa walinyanyaswa kingono kupitia maneeo ikilinganishwa na asilimia 33 .

Na asilimia 20 ya wanaume nchini Iraq walisema kuwa walinyanayswa kingono kupitia maungo na maneno ikilinganishwa na asilimia 17 ya wanawake wa Iraq.

Wanaume wengi wa Iraq pia walisema kwamba walikuwa wakishambuliwa nyumbani.

Haya ni matokeo ya kushangaza, kutokana na hali ya haki za kibinadamu za wanawake katika taifa hilo .

Kifungu cha 41 cha sheria nchini Iraq kinasema kuwa sio haramu kwa mwanamume kumpiga mkewe.

Hatahivyo Dkt Kathrin Thomas mtafiti wa maswala ya ulimwengu wa kiarabu ambaye alifanya utafiti huo ameonya kwamba huenda wanawake hawaripoti visa vya kunyanyaswa na wameamua kunyamaza kinya.

Image caption

Maisha ya sami yaliimarika baada ya kuhamia Baghdad


Utafiti wa BBC.

  • Zaidi ya watu 2500 walihojiwa katika mataifa ya mashariki ya kati na kaskanzi mwa Afrika – Algeria, Misri, Iraq, Jordan, Kuwait, Lebanon, Morocco, Sudan, Tunisia, na Yemen – na maeneo ya Palestina .
  • Huu ni utafiti mkubwa kwa idadi ya watu waliohojiwa katika baadhi ya mataifa na ukiwa wa kina zaidi kulingana na maswali yalioulizwa.
  • Ulifanywa na shirika la Utafiti la Arab Barometer, lililopo katika chuo kikuu cha Princeton University

Anakumbuka mambo aliyokabiliana nayo akiwa shule akia na umri wa miaka 13 wakati alipolaumiwa kuwa mwathiriwa wa shambulio na anasema kisa kama hicho kinaweza kutokea temna.

Iwapo ningelalamika kuhusu kubakwa kwa maafisa wa polisi – maafisa hao hawataniona mimi kama mwathiriwa bali pia wanaweza kunipeleka jela kwa kuwa nitaonekana kuwa mshirika wa kisa hicho – cha usenge – ambacho ni haramu , anasema.

Sheria inaniunga mkono lakini wale wanaoshinikiza sheria hiyo kufuatwa hawaniungi mkono.

Msemaji wa maafisa wa polisi wa Iraq anasema kuwa katika taarifa kwamba : Milango yetu iko wazi kwa raia. Wanyanyasaji wa kingoni wamekamatwa baada ya waathiriwa kuripoti .

Taarifa hiyo inasema kwamba mpango mpya umeafikiwa 2003 sambamba na uelewa wa taifa hilo wa haki za kibinadamu na kwamba maafisa maalum wameajiriwa kukabiliana na visa kama hivyo

Sami ana umri wa miaka 21 sasa.

Maisha yameimarika sasa . Anapenda kuishi mjini Baghdad.

Anafanay kazi katika shirika kubwa la kimataifa pamoja na kundi la maraifiki zake ambalo linaelewa maisha yake ya zamani.

Anatumai kwa kuelezea hadithi yake BBC atawarai wanaume wengine kuzungumzia matatizo yao.Source link