Uongozi wa harmonize umefunguka kuhusu kudaiwa msanii wake Harmonize kuiba wimbo UNO kutoka kwa msanii Kenya.

“Kupitia ukurasa wake wa Instagram Meneja huyo wa Harmonize Mjerumani kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika haya:-

Tumepata Taarifa kutoka Youtube Kwamba,mtu mmoja ambae Inasemekana Kutoka Nchi jirani Kenya,Ametuma Barua pepe kudai umililiki wa wimbo wetu Pendwa #UNO.
Aidha kwa taratibu zao YouTube Ni Lazima wauweka Private wakati wakiendelea na taratibu za Kujirdhisha juu ya madai hayo.

Tunachukua Nafasi hii Kuwaomba Mashabiki wetu na wapenzi wa Harmonize,Kuwa Watulivu Wakati jambo hili linashughulikiwa. Aidha Tunaimani Wimbo wetu Utarudi baada ya muda sio mrefu.Tunawashukuru kwa sapoti yenu.Mungu Awabariki.Asanten sana.
BY HARMONIZE MANAGEMENT #AfroEast #UNO”

By Ally Juma.

Source link