Members of the MEK at their new base in AlbaniaHaki miliki ya picha
Getty Images

Kwa miaka sita, Albania kumekuwa ni nyumbani kwa kikundi kimoja cha makundi makuu ya upinzani nchini Iran, linalojulikana na kama Mujahideen-e-Khalq, au MEK.

Wakini mamia ya wafuasi wa kundi hilo wamejiondoa- baadhi wakilalamika kuwa sheria kali za kundi hilo zinazowalazimisha kuwa waseja, na kudhibiti mawasiliano ya familia zao.

Kwa sasa makumi kadhaa wanaishi katika mji mkuu wa Albanian, Tirana, wameshindwa kurejea Iran au kuweza kurejea katika hali ya maisha ya kawaida.

“Sijaweza kuzungumza na mke na mtoto wangu wa kiume kwa miaka zaidi ya 37 walikuwa wanafikiri nilikufa. Lakini niliwaambia, ‘Hapana ninaishi, ninaishi Albania…’ Walilia.”

Mawasilia hayo ya kwanza kwa njia ya simu na familia yake baada ya miaka mingi sana yalikuwa magumu pia kwa Gholam Mirzai.

Ana umri wa miaka 60, na alitoroka kutoka kwenye kikundi hicho miaka miwili iliyopita katika jeshi lake lililopo nje ya mji wa Tirana.

Sasa amekwama katika mjini mkuu wa Albania, akiwa mwenye majuto na akishutumiwa na wapiganaji wenzake wa zamani wa Mujahideen kuwa ni jasusi wa adui zao, serikali ya Jamuhuhuri ya kiislamu ya Iran.

Kundi la wanamgambo (MEK) linana histolia ya mtikisiko na umwagaji damu. Likiwa ni kundi la Waislam wenye itikadi kali za Kimarxist , wajumbe wake waliunga mkono mapinduzi ya Iran ya 1979 yaliyomg’oa madarakani Shah. Lakini mahusiano na Ayatollah Khomeini yaliharibika baada ya muda mfupi. Wakati serikali ilipoanza kuwasaka na kuwakamata Mujahideen walilazimika kukimbia nchi kulinda maisha yao.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

MEK members being rounded up in Tehran in 1982

Nchi jirani ya Iraq iliwapatia maficho, na kutoka kwenye eneo la lao mwinuko la jangwani wakati wa vita vya Iran/Iraq vya mwaka (1980-1988), MEK walipigana upande wa Saddam Hussein dhidi ya nchi yao Iran.

Gholam Mirzai alikuwa akihudumu katika jeshi la Iran wakati alipokamatwa na vikosi vya Saddam Hussein katika mwanzo wa mzozo huo. Aliishi miaka minane gerezani kama mfungwa wa vita nchini Iraq . Lakini wakati huo, wafungwa wa Iran kama Mirzai walikuwa wanashawishiwa kujiunga na jeshi na Wairan wenzao . Na hilo ndilo alilolifanya.

Mirzai sasa “amejitenga nao ” – akiwa ni mmoja wa mamia ya wajumbe wa zamani wa MEK ambao waliondoka katika kundi hilo tangu walipohamia Albania. Kwa usaidizi wa pesa kutoka kwa familia zao baadhi wamewalipa wafanyabiashara haramu ya binadamu kuwapeleka katika maeneo ya Ulaya, na huenda baadhi wameweza kurejea nyumbani elsewhere in Europe, and perhaps two have made it back to Iran. Lakini makumi kadhaa bado wamekwama katika mji wa Tirana, wakiwa hawana utaifa na hawawezi kufanya kazi rasmiNi vipi mapigano yaliwawezesha wajumbe wa kundi la MEK- ambao zamani walielezewa kama shirika la ugaidi katika mataifa ya Marekani na Ulaya – kuingia katika eneo hili la Ulaya?

Mnamo mwaka 2003, uvamizi wa jeshi la Muungano unaoongozwa na Marekani nchini Iraq kuliyafanya maisha ya MEK mahsakani. Mlinzi wa kundi hilo , Saddam Hussein, aliondoka ghafla, na Mujahideen walishambuliwa mara kwa mara- mamia wakafa na wengine kujeruhiwa. Kwa kuhofia maafa makubwa zaidi, Marekani ikawasiliana na serikali ya Albania mwaka 2013 na ikaishawishi kuwapokea wajumbe 3,000 wa MEK m mjini Tirana.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wapiganaji wa kike wa MEK wakifanya mafunzo ya kijeshi wakati wa vita vya Iran na Iraq (1984)

“Tuliwapatia hifadhi ili kuwakinga na mashambulio na unyanyasaji, na uwezekano wa kuishi maisha ya kawaida katika nchi ambako hawakunyanyaswa, kushambuliwa na kufanyiwa ukatili ,”anasema Lulzim Basha, kiongozi wa chama cha Kiddemokrasia, ambacho kilikuwa mamlakani wakati huo, ambaye sasa yuko katika upinzani.

Nchini Albania, siasa inashabikiwa sana- kila kitu kinagombewa kwa uchaguzi. Lakini, hali ya kisiasa huko ni ya kipekee, uwepo wa MEK si wazi, serikali na upinzani wanawaunga mkono wageni hao kutoka Iran.

Kwa wajumbe wa MEK, Albania yalikuwa ni mazingira mapya kabisa. Gholam Mirzai alishangazwa na kwamba hata watoto walikuwa na simu za mkononi. Na kwasababu baadhi ya Mujahideen walikaribishwa mwanzo katika nyumba za gorofa viungani mwa mji mkuu, ukaribu wa kundi hilo na wajumbe wake ulipungua kuliko ilivyokuwa awali.

Nchini Iraq, lilikuwa limedhibiti karibu kila sekta ya maisha , lakini hapa, lilikuwa na fursa japo ya muda mfupi la kuisha maisha huru kwa kiwango fulani.

“Kuna uwanja mbaya nyuma ya magorofa ambapo makamanda walituambia tunapaswa kuutumia kufanya mazoezi ,”anakumbuka Hassan Heyrany, mjumbe mwingine “aliyejitenga ” na MEK

Heyrany na wenzake walitumia matawi ya miti na vichaka kujificha na kuingia kwenye vituo vya intaneti na kufanya mawasiliano na familia zao.

“Tulipokuwa nchini Iraq, kama ungetaka kupiga simu nyumbani MEK walikuita dhaifu- hatukuwa na uhusiano na familia zetu ,” alisema. “lakini tulipokuja Tirana, tulipata intaneti kwa ajili ya matumizi ya kibinafsi.”

Image caption

Hassan Heyrany sasa

Karibu na mwisho wa mwaka 2017, hata hivyo MEK walitoka nje ya makao makuu. Kambi ilijengwa katika eneo la mlima uliopo maeneo ya vijijini nchini Albania, karibu kilomita 30 (maili 19 ) kutoka mji mkuu.

Nyuma ya lango la chuma la kambi hiyo kulikuwa na sanamu ya dhahabu ya simba. Kulikuwa na miti iliyopandwa kwa mistari kuelekea katika eneop la makumbusho ya maelfu ya watu waliopoteza maisha yao katika mapambano ya MEK’s dhidi ya serikali ya Iran.

Waandishi wa habari wasio na mwaliko hawapokelewi hapa . Lakini mwezi Julai mwaka huu, maelfu walihudhulia tukio la MEK la Iran hutu katika kambi hiyo. Wanasiasa kutoka maeneo mbali mbali ya dunia , Waalbania wenye ushawishi na wakazi wa kijiji jirani na kambi cha Manze, walijiunga na maelfu ya wajumbe wa MEK na kiongozi wao , Maryam Rajavi. Wakili binafsi wa rais wa Marekani Donald Trump , Rudy Giuliani, alihutubia umati wa watu waliohudhuria tukio hilo.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Rudy Giuliani: “Kama unafikiri hii ni kundi haramu la imani ya kishetani una kasoro”

“Hawa ni watu waliojitolea kwa ajili ya uhuru,” alisema, akimaanisha wajumbe wa MEK waliokuwa wamevalia sare ya kijeshi waliokuwa wamejipanga wanawake na waume katika mistari tofauti.

“Na ”Kama unafikiri hii ni kundi haramu la imani ya kishetani una kasoro”,” aliongeza, na wajumbe wa MEK na waliohudhuria tukio hilo wakampigia makofi.

Wanasiasa wenge mamlaka makubwa kama Giuliani wanaunga mkono lengo la MEK la kuleta mabadiliko nchini Iran. Sera ya vuguvugu hilo ni pamoja kuleta haki za binadamu , usawa wa jinsia, na demokrasia shirikishi nchini Iran.

Lakini Hassan Heyrany haamini hilo tena. Mwaka jana aliondoka katika kikundi cha MEK, akipinga kile alichokiona kama udhibiti waukandamizaji wa uongozi wa MEK wa maisha yake.

“Ilikuwa inavutia sana. Lakini kama unaamini demokrasia , hauwezi kukandamiza mioyo ya wajumbe wako ,” anasema.

Haki miliki ya picha
Hassan Heyrany

Image caption

Hassan Heyrany nchini Iraq mwaka 2006

“Mahaba na ndoa vinazuiwa na MEK. Haikuwa hivyo kila siku – wazazi na watoto wao walikuwa wanajiunga na Mujahideen.

Lakini baada ya kushindwa vibaya katika moja ya uvamizi wa Iran , viongozi wa MEK walidai kuwa kushindwa kwao kumetokana na kwamba mahusiano ya kibinafsi ya Mujahideen ambayo yaliwafanya wasiwe makini katika vita.

Talaka nyingi zilifuatia. Watoto wakapelekwa mbali – mara kwa mara walipelekwa katika nyumba za walezi barani Ulaya na wajumbe wa MEK ambao hawajaoa wakaahidi kuishi maisha ya useja. Mfano kama ningekuwa na hisia za ngono , nilipaswa kuandika kwenye kijidaftari kuwa ” Leo nimepatwa na msisimko wa ngono”

Katika vijidafrali hivyo, Heyrany anasema pia walilazimika kuandika ndoto zao za mchana.

Unaweza pia kusoma:

  • Vita kati ya Iran na Marekani ‘haitatokea’
  • Msomi wa Uingereza na Iran akamatwa

“Kwa mfano, ‘Nilipomuona mtoto mchanga kwenye televisheni, nilikuwa na hisia ya kuwa na mtoto au familia yangu mwenyewe .'”

Na Mujahideen walipaswa kusoma yaliyoandikwa kwenye vijitabu hivyo mbele ya kamanda na wenzao katika mkutano wa kila siku.

“Hilo ni jambo gumu sana kwa mtu,” Heyrany anasema.

Chanzo cha kidiplomasia mjini Tirana kililielezea kundi la MEK kama “kikundi cha kipekee cha kitamaduni – na sio kikundi chenye imani za kishetani, bali linalofanana na la kitamaduni.”

BBC haikuweza kubaini lolote la aina hii katika kikundi cha MEK , kwasababu kundi hilo lilikataa kuhojiwa. Lakini nchini Albania, nchi ambayo ilipitia kipindi cha adhabu, kufungwa, utawala wa kikomunisti kwa miongo kadhaa, kuna msimamo wa huruma kwa uongozi wa MEK – walau juu ya marufuku ya mahusiano ya kibinafsi.

“Katika hali ambazo ni mbaya sana, unafanya maamuzi magumu,” anasema Diana Culi, mwandishi wa vitabu, mwanaharakati wa wanawake na mbunge wa zamani katika serikali ya chama tawala cha kisoshalisti.

“Waliapa kupigana maisha yao yote kwa ajili ya ukombozi wa nchi yao kutoka kwa utawala wa Iran. Wakati mwingine inakuwa vigumu kwetu kukubali imani kali kwa ajli ya lengo fulan . Hii ni kujitolea binafsi na naelewa ni suala la kuamini kiakili .”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Female guards at the MEK headquarters in Albania

Lakini licha ya hayo, baadhi ya Waalbania wanahofia usalama wao kutokana na uwepo wa MEK.

Wanadiplomasia waili wa Iran walifukuzwa nchini humo kufuatia madai juu ya kupanga njama za mashambulio dhidi ya Mujahideen, na Muungano wa Ulaya umeishutumu serikali ya Tehran kwa kuwa nyuma ya mpango wa kuwaua wapinzani , wakiwemo wajumbe wa MEK, katika ardhi za Uholanzi, Denmark na Ufaransa . (Ubalozi wa Iran mjini Tirana ulikataa ombi la BBC la kufanya nao mahojiano.)

Chanzo kinachoaminika katika chama cha Kisoshalisti pia kinaeleza kwamba huduma za ujasusi hakina uwezo wa kufuatilia wajumbe wa MEK zaidi ya 2,500 MEK wenye mafunzo ya kijeshi nchini humo.

“Hakuna mtu yeyote mwenye akili angewakubali hapa ,” anasema.

Wakati Mirzai alipoondoka kwenda katika vita dhidi ya Iraq mwaka 1980, alikuwa na mtoto wa kiume wa mwezi mmoja. Baada ya vita vya Iraq na Iran vilipomalizika, mke wake na ndugu zake walikuja katika kambi ya MEK nchini Iraq kumtembelea Mirzai. Lakini MEK iliwafukuza, na haikumwambia lolote kuwahusu.

Mirzai mwenye umri wa miaka 60- hakujua kuwa alikuwa anapendwa na kukumbukwa na mwanae na mkewe hadipale alipopiga simu nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 37.

“Hawakuniambia kuwa familia yangu ilikuja kunitafuta Iraq. Hawakuniambia lolote kuhusu mke wangu na mwanangu,” anasema.

” Miaka yote hii nimekuwa nikimfikiria mke na mwanangu. Labda walikufa vitani… Sijui .”

Haki miliki ya picha
Hassan Heyrany

Image caption

Gholam Mirzai akiwa Tirana sasa

Mwanae ambae hajamuona uso kwa uso tangu alipokuwa mtoto mchanga miaka karibu 40 sasa. Na Mirzai anajivunia kuonyesha picha ya kijana wake kwenye WhatsApp ambaye sasa ni mtu mzima. Lakini pia mawasiliano mapya yamekuwa na maumivu yake pia.

“Niliwajibika kwa hali hii ya kutengana . Siwezi kupata usingizi wa kutosha kwasababu ninawafikiria. Nina aibu wakati wote na hasira . Ninajionea aibu mwenyewe ,” anasema Mirzai.

Aibu sio kitu rahisi kuishi nacho. Na sasa anatamani kitu kimoja tu.

“Ninataka kurudi Iran, kuishi na mke wangu na mwanangu. Hicho ndicho ninachokitaka .”

Gholam Mirzai mekwishatembelea ubalozi wa Iran mjini Tirana kuomba msamaha, na familia yake imefanya mipango na maafisa wa Tehran kujaribu kumrejesha Mirzai . Hajapata jibu lolote. Kwahiyo anasubiri-bila uraia, bila paspoti, lakini ana ndoto ya kurudi nyumbani .Source link