Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amebainisha kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Lori liligonga treni.
Treni hiyo iliyokuwa inatoka Tabora kwenda Dar es Salaam ilipata ajali kabla ya kuingia stesheni ya Dodoma na kuanguasha mabehewa yake matatu, Kw3a mujibu wa Mwananchi digital, Ajali hiyo imetokea jana saa 5.30 usiku.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, @patrobas_katambi_ ameeleza leo asubuhi kuwa ajali hiyo imetokea saa 5.30 usiku.

Amesema ametoa maagizo kadhaa ikiwemo kumsaka dereva wa lori ambaye inasemekana aliruka kutoka kwenye lori baada ya ajali hiyo.
Tutawaletea taarifa zaidi kutoka Mamlaka husika.

By Ally Juma.

 

Source link