Kapteni Mstaafu George Mkuchika Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amekemea vikali vitendo vinavyoendelea kwa sasa ambavyo vimekithiri katika jamii zetu vya ubakaji na kuwalawiti watoto wadogo wenye ndoto za kufika mbali huku wakiwa hatarini kupata magonjwa kama Ukimwi.

Lakini pia amewataka TAKUKURU kufuatilia kwa ukaribu rushwa ya ngono hasa inavyoendela Vyuoni lakini p[ia kuwaonya vikali Wazazi wanaoonyesha ushirikiano na watru wanaofa vitendo hivi. ” Wazazi ambao Mwanao anaingiliwa mnanyamaza au mnamalizana na Mtuhumiwa ole wenu tutakupeleka wewe baba mzazi na huyo aliyefanya hicho kitendo”

Mbali na hivo Waziri Mkuchika ameongeza kuwa “Mungu katujalia nchi inawanawake wengi na wazuri na wanavaa vizuri oa hata kumi hakuna atakayekuuliza mbona umewachukua wanawake wengi, Nasikia Wenzangu waislamu hapa mnaruhusiwa nimeambiwa mpaka wanne lakini najua hapa mnazidisha, mie naitwa George na wenzake tumeambiwa mmoja haya tukifanya ukaguzi hapa wale wengine? kwanini uhangaike na Watoto?”

Video Credit by Ngasa tv.

By Ally JumaSource link