Kufuatila Kautli kauli aliyoitoa siku jana kuhusu nchi ya Rwanda kuingia mkataba na klabu ya PSG kutoka Ufaransa kwa ajili ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini Rwanda kitu kilichopelekea Watanzania kuanza kuitupia lawama Wizara husika hapa nchini, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.

Hamisi Kigwangalla aliamua kutoa taarifa fupi kuhusu kiachoendelea kati ya wizara yenye dhamana na baadhi ya timu kutoka nje ya nchi ambazo tayari zimetuma maombi ya kuingia mkataba na Tanzania kwa ajili ya kuutangaza utalii wetu na haya ndio yalikuwa maneno ya Waziri Kigwangalla:-

“Nimekuwa nikipokea malalamiko na ushauri mwingi kufuatia ndugu zetu wa Rwanda kusaini dili na @PSG_English. Tunafahamu nguvu na nafasi ya soka ya ulaya kwenye kutangaza brands. Tanzania tumefuatwa na vilabu kadhaa, bado tunachambua kabla Serikali haijaamua kama tuingie ama la. #TanzaniaUnforgettable,”

Baada ya Watanzania kuanza kulalamika na kusema Wizara inaiga mambo kutoka Rwanda Waziri mwenye dhamana aliamua kuutumia ukurasa wake wa Twitter na kuandika haya.

By Ally Juma.

Source link